EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, October 17, 2013

KENYA YATUMA VIKOSI MAALUM KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA



RAIS UHURU KENYATA WA KENYA

Serikali ya Kenya imetuma vikosi maalum vitatu, kupambana na hali ya kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kulevya, na uwepo wa silaha haramu, vinavyoathiri vijana wasiokuwa na ajira katika sehemu ya kaskazini mwa Kenya. Hatua ya serikali inatokana na wasiwasi waliouonesha wazee wa kikabila katika sehemu ya kaskazini mwa Kenya, waliosema matatizo hayo yanachangia kuvuruga usalama katika sehemu ya kaskazini mwa Kenya.


Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na tatizo la kuongezeka kwa uhalifu katika eneo la Bungoma, ambako watu 30 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika eneo la Trans Nzoia watu 15 waliuawa, ikiwa ni pamoja na polisi watatu.Watu hao waliuawa na majambazi walionunua silaha haramu kutoka Uganda.Tatizo la umasikini na ukosefu wa ajira yanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la uhalifu katika sehemu mbalimbali za Kenya.

No comments:

Post a Comment