Mtu mmoja jana alisema sasa hivi wasafiri watokao Tanzania
wanakaguliwa kwa makini zaidi ya ilivyokuwa hapo awali kutokana na
matukio ya kukamatwa na dawa za kulevya! Hii ni sifa mbaya mno kwa raia
na Taifa zima!Iliyopachikwa hapo chini ni taarifa kutoka kwenye tovuti ya Serikali ya Hong Kong ya Julai 26, 2013
Hong Kong Customs yesterday (July 25) detected three drug trafficking
cases, with seizures totally valued at $4.78 million, in the
department's escalated anti-narcotics efforts to combat drugs. Customs
officers at the Hong Kong International Airport (HKIA) intercepted a
26-year-old incoming...
HAUSIBOI ALIYEMLAWITI BINTI WA MIAKA MINNE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA HUKO MPANDA
Mahakama
ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu kijana,
Baraka Juma (22) mkazi wa kijiji cha Nkungwi wilayani humo, kifungo
cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumlawiti
mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne baada ya kumhadaa na
kumlewesha bia.
Akisoma
hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga
Tengwa alisema ameridhishwa na ushahidi pasipo kutia shaka
uliotolewa mahakamani hapo na upande zote mbili za mashitaka na
utetezi.
“Nimelazimika...
MBUNGE NASSARI ASOTA POLISI KWA MADAI YA KUMPIGA KADA WA CCM
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari jana
alishikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha kwa saa tatu na nusu kwa
tuhuma za kumshambulia kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein
Warsama siku ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni, wilayani
Monduli.
Nassari
aliyefika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha saa 2:30 asubuhi jana ili
kuitikia wito wa kutakiwa kuripoti kituoni hapo, alinusurika kuswekwa
mahabusu baada ya kujidhamini mwenyewe majira ya saa saa 6:02 mchana na
hivyo kuachiwa kwa dhamana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha (RCO), Nassari
anadaiwa kumshambulia Warsama...
VIDEO YA MWANACHUO AKIKATA MAUNO NUSU UCHI....
Katika hali isiyo ya kawaida, mwanafunzi mmoja wa kike wa chuo
kikuu maarufu hapa nchini ametoa kali ya mwaka baada ya kuamua
kupiga chini kitabu na kuanza kukata mauno huku akiwa na
kikanga kimoja kiuoni na sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa
wazi hasa matiti....Video iko hapo chini:
<<VIDEO IKO HAPA>>...
PROGRAM YA AJIRA KWA VIJANA WALIOHITIMU VYUO VIKUU NCHINI....
PROGRAMU YA AJIRA
Programu hii itatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu
ya juu nchini,Taasisi za fedha na wabia wa maendeleo.Kwa kuanzia
utekelezaji wake utaanza kwa kuendeleza programu ya mfano iliyoanzishwa
na Idara ya kilimo, uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (DAEA-SUA) na hatimaye kuwafikia wahitimu wa vyuo vingine vya
elimu ya juu katika kipindi husika.
Kwa kuanzia serikali imekubaliana na Benki ya CRDB kuanza utoaji wa
mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa programu utakapoanza.
Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya juu nchini imeongezeka wastani wa
(48% kwa mwaka) na Wizara imeona...
USABATO WADAIWA KUKIANGAMIZA CHUO CHA AURUSHA (UoA)
Haya ni malalamiko ya mdau anayesimulia jinsi USABATO
unavyokiangamiza chuo cha Ausha...
Katika maelezo yake aliyoyatoa mzalendo forum, mdau huo anaripoti
kuwa bila kuwa msabato huwezi kuajiriwa chuoni hapo, bila kuwa
msabato huwezi kushinya uongozi wowote wa wanafunzi.....
Je kuna ukweli wowote???
HUU NDO UJUMBE WAKE
<<USABATO WA CHUO CHA ARUSHA>&...
VIDEO: ANGALIA NAMNA BAYERN MUNICH WALIVYOPIGWA 4-2 NA DORTMUND KATIKA MECHI YA KUFUNGUA MSIMU WA BUNDESLIGA
Dortmund imeifunga Bayern Munich 4-2 katika mchezo wa Supercup uliochezwa leo. |
HIVI NDIVYO TAIFA STARS ILIVYONYOLEWA NA UGANDA THE CRANES NA KUSHINDA KWENDA CHAN
Wachezaji wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na Uganda Cranes wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mechi yao ya kufuzu kucheza Chan iliyofanyika kwenye uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala. |
Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes'
|
Mchezaji
wa Taifa Stars Aggrey Morris (katikati) akiwania mpira huku akizongwa
na mabeki wa Uganda Cranes.Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager.
|
Amri Kiemba akipongezwa na Mrisho Ngasa/ Aboubakar Salum 'Sure Boy' baada ya kushinda bao la kusawazisha dhidi ya Uganda Cranes |
Washabiki wa Taifa Stars wakishangilia goli la kusawazisha..
|
Kiemba |
HATIMAYE TAIFA STARS WATOLEWA CHAN - WAPIGWA 3-1 NA UGANDA THE CRANES
Tanzania
(Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa
Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka
huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya
mabao 4-1.
Stars
ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009
ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao
1-1.
Wenyeji
ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo
iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda
alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la
Tanzania.
Bao
hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na
kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana
na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.
Dakika
ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho
Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba
kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.
Mabao
mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian
Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na
makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi
nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha
Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva
badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo
Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John
Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi
cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David
Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd,
Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo,
Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho
(Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.
No comments:
Post a Comment