MZIMU wa serikali tatu bado unaendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), ambapo jana, Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
alipinga tena uwepo wa serikali tatu na kudai kuwa waliotoa maoni hayo
ni wazee wanaosubiri kufa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika
kongamano la Umoja wa Vijana (UVCCM) la kujadili mchakato wa Katiba
Mpya, katika ukumbi wa Arnatouglo, Nnauye alisema nia ya serikali tatu
ni kuleta matabaka ambayo yatasababisha migogoro.
“Wazee hawa wanaosubiri kufa wanataka kutuletea matabaka, vijana
ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha kuwepo kwa serikali tatu ni
kusababisha mgogoro, kwa nini wasingevunja...
"SASA NIMEOKOKA.....UJINGA SITAKI TENA"...LULU MICHAEL
MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema
baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza
katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake.
Lulu alisema hayo juzi,
katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha
Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.
“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya
kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.“Ningependa
maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu
labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi
baadaye,” alisema Lulu.Katika...
RAIS PAUL KAGAME HATARINI KUSHITAKIWA ICC
ONYO lililotolewa na Ikulu ya Marekani dhidi ya Serikali ya Rwanda,
linalomtaka Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame, kuacha kuwasaidia waasi wa
kikundi cha M23, lina kila dalili zinazomuweka kwenye kundi la viongozi
wa Kiafrika ambao hatma yao baada ya kuachia madaraka inazungukwa na
wingu la mashaka.Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye mapema
wiki hii alikaririwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani akimtaka
Rais Kagame kuacha kukisaidia kijeshi kikundi cha waasi wa M23,
anaaminika kuitoa kauli hiyo kama msimamo wa serikali yake inayopinga
watawala wanaojihusisha na uhalifu wa kivita.Ingawa hadi sasa
Rais Kagame hajatajwa na Ikulu...
No comments:
Post a Comment