EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, July 9, 2013

UGOMVI WA NDOA WASABABISHA MWANAMKE AVAMIWE NA KUKATWA MIKONO YAKE


Mwanamke mmoja Sumayi Girandi mkazi wa kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda amepoteza vidole vitatu vya mkono wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto kukatwa baada kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana kisa kikidaiwa kuwa kutaka kunyang’anywa mali zake. Uhodari wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na kisha  wakamkata kiganja cha mkono wa kushoto na kuanguka. Kwa sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya. Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake...

BONDIA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU......ALIKUWA AKIAMULIA UGOMVI KABLA YA KISANGA KUMGEUKIA

BONDIA  maarufu Ramadhani Idd ‘Mashudu’ ameuawa kwa kuchomwa visu mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lililowaacha midomo wazi wakazi wa Mabibo Loyola, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam lilitokea saa sita usiku Julai 4, mwaka huu. Imedaiwa kuwa, marehemu aliwakuta Jack Mchaki na mtu mwingine wakigombana, alipowaamulia wakamgeuzia kibao na kumchoma visu. Waandishi wetu walifika eneo la tukio na kukutana na mashuhuda waliozungumza kwa sharti la kutoandika majina yao , mmoja alidai marehemu alikuwa anaangalia kanda za filamu katika banda moja maeneo hayo ghafla alifika Jack aliyelewa na kuanza kufanya fujo. Shuhuda...

GIZA LATANDA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO....MSIMU WA MASOMO UMEANZA HUKU "SELECTION" ZIKIWA BADO

Matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka 2012, yameendelea kuitikisa sekta ya elimu nchini baada ya shule kufunguliwa jana bila kutangazwa kwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu. Kwa kawaida, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu, hutangazwa mapema ili kutoa fursa kwa wanafunzi na shule husika kufanya maandalizi ya mahitaji. Lakini tofauti na ilivyozoeleka, wanafunzi wa kidato cha sita walianza masomo yao jana huku wale wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu wakiwa hawajatangazwa. ...
TUPE MAONI YAKO

MBUNGE WA DODOMA MJINI AWATEMBELEA WAHANGA WAMLIPUKO WA PETROL KATIKA HOSPITAL YA MKOA WA DODOMA

Mbunge wa Dodoma mjini  Mh Dr David Mallole, alipoenda kuwatembelea wahanga wa mlipuko wa Petrol katika hospital ya mkoa wa Dodoma,General Hospital na kutoa pole kwa wagonjwa waliopatwa na janga hilo kwa kuwapatia pole pamoja na msaada wa pesa ya dawa kwa kila mmoja Mtoto huyu ni mwanafunzi wa kidato cha tatu Shabani p. Shaban .Alikutana na janga hili baada ya kwenda kwa fundi kuchukua nguo zake za shule ambapo ni eneo jirani na mlipuko huo ulipotokea. Mh Mbunge David Mallole ameahidi kumlipia ada yake ya shule: Credit: Bossngasa blog...
TUPE MAONI YAKO

HUDUMA YA TRENI LA JIJI KESHO HAIPO....KICHWA KIMOJA NI KIBOVU

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na wakazi wa jiji kwa jumla kuwa huduma ya treni ya jiji haitokuwepo kwa muda wa siku 2 kuanzia leo Julai 8, 2013 kutokana na hitilafu kubwa katika  kichwa kimojawapo cha treni hiyo.Uamuzi huo unatokana na sababu za kiufundi unaosimamia uendeshaji wa huduma hiyo jijini. Kwa utaratibu huduma hii huendeshwa kwa kutumia vichwa vya treni vitatu ambapo viwili uhudumia moja kwa moja na cha tatu huwa cha akiba .  Kuanzia siku ya Jumamosi ambapo huduma haikuwepo, kichwa cha  tatu kiligundlika kuhitaji matengenezo makubwa na kupelekwa katika karakana yetu ya Morogoro. Kutokana na utaratibu tulioainisha hapo awali kukosekana kichwa cha dharura ’standby’ kunalazimisha tusitishe huduma kwa muda. Hata...
TUPE MAONI YAKO

SABABU TANO ZILIZOWAFANYA CHADEMA WAGOME KUSHIRIKI "KONGAMANO LA AMANI" LINALOANZA KESHO

Ndugu waandishi wa habari,Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharula, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).Kongamano hilo linatajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.Baadhi...
TUPE MAONI YAKO

VIDEO: JENGO LA WIZARA YA UCHUKUZI LIMENUSURIKA KUUNGUA MOTO

Shughuli za serikali zimelazimika kusimama kwa zaidi ya saa moja kutokana na wafanyakazi wa wizara ya uchukuzi kukimbia nje ya ofisi zao baada ya jengo lililoungana na wizara hiyo kupata hitilafu ya umeme iliyosababisha kutaka kuanza kuungua moto...
TUPE MAONI YAKO

UWOYA AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUMFANANISHA DIAMOND NA MICHAEL JACKSON

Mwigizaji  wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson. Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.  Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.  “Sasa...
TUPE MAONI YAKO

"PREZZO ANAYAJUA MAPENZI.....HATA AKINIUTHI SITAHESABU MAKOSA YAKE"....DIVA WA CLOUDS FM

Muda mfupi uliopita mtangazaji wa ‘Ala za Roho’ ya Clouds FM Diva Loveness Love ambaye sasa anatumia “divathebawse” katika akaunti yake ya Instagram, ameweka picha mpya akiwa na Rapcellency Jackson makini aka Prezzo kutoka Kenya waliyopiga jana (July 7). Picha hiyo ambayo inawaonesha wawili hao wakiwa “0 distance” ilikuwa na caption inayosomeka hivi, “Nothing Than Happiness… Prez is such a Nice guy. Hata Akiniudhi Sihesabu makosa yake. May you Live Long Pleaseeee……… Good hearted, My hero, My Mentor… A Person I can count to when I need to be happy… No one is Perfect yes but I love his flaws and All…. Bless you always’ . I Pray you...
TUPE MAONI YAKO

UGONJWA WA KIPINDUPINDU WALITIKISA JIJI LA MBEYA...MIKUSANYIKO YAPIGWA MARUFUKU

  UGONJWA wa kipindupindu, umeingia katika wilaya ya Kyela na kuua watu wawili na 39 wakiwa wamelazwa.Taarifa zinasema ugonjwa huo umeibuka wilayani humo wiki iliyopita ukisadikika kuanzia katika Kijiji cha Ngonga na kisha kusambaa hadi Kilwa.Kutokana na hofu ya kupata maambukizi kwa wananchi wengine, serikali imepiga marufuku mikusanyiko ikiwemo ya harusi, kipaimara, ngoma, michezo na sikukuu inayosherehekewa kila mwaka ya wakulima. ...
TUPE MAONI YAKO

ANGALIZO:MAFUTA YA UBUYU YANA TINDIKALI INAYOSABABISHA SARATANI

Baada ya kuonya wananchi wanaotumia dawa za tiba mbadala ambazo hazijathibitishwa, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), sasa inawataka wananchi kuacha kutumia mafuta ya ubuyu kwa kunywa kama dawa. Akizungumza juzi katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema Mamlaka hiyo ilipima na kubaini mafuta hayo yana tindikali ya mafuta.  Alifafanua katika maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, kwamba mafuta hayo hayafai kuliwa na binadamu na anayekunywa kwa wingi, yuko hatarini kupata saratani za aina tofauti tofauti....

No comments:

Post a Comment