EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, February 27, 2014

MTWARA SASA HATARI WANANCHI WAMWAGIWA SUMU MBAYA NA KAMPUNI YA SBS



Mornitoring/ Mdenga.
Reporters/ Mohamedi & Aloyce.
 Wakazi waishio katika mtaaa wa Mdenga Mkoani Mtwara waiomba serikali kuhamisha au koboresha mazingira ya dampo la kuchomea sumu la SBS ili kuepukana na adha ambazo wamekuwa wakizipata kutokana na uwepo wa dampo hilo.

Hayo yamezumgumzwa mapema hii leo na wakazi hao wakati wakizungumza na waandishi wa habari wa Pride Fm Radio katika eneo hilo.

Mmoja wa wakazi hao Ayubu Rashidi amesema wamekuwa wakipata adha mbalimbali kutokana na uwepo wa dampo hilo ikiwemo ya harufu kali na maradhi ya kifua yanayotokana na moshi wenye kemikali za sumu.

Pia Subira Ndege ni mmoja wa wakazi waishio eneo hilo amesema kuwa kutokana na dampo hilo kutililisha maji machafu yenye sumu katika dimwi la maji ambayo wamekuwa wakiyatumia katika maisha yao ya kila siku wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali yakiwemo ya kuwashwa mwili pindi watumiapo maji hayo.

                                     

No comments:

Post a Comment