Rais Obama kuzuru Afrika; kukaa Tanzania siku mbili
Rais
wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika Kusini na
Tanzania mwezi Juni. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya White
house.
Rais Obama atakutana na watunga sheria na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa asasi za kijamii.
Alizuru
Ghana mwaka 2009 .Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni hadi 3 Julai na
itakuwa ziara yake ya pili Kusini mwa jagwa la Sahara akiwa rais wa
Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na mwenzake George W Bush, wote walizuru Afrika wakati wa muhula wao wa pili wa utawala.
Clinton alizuru nchi sita wakati Bush akizuru nchi tano.
''Rais
atatilia mkazo uhusiano kati ya Marekani na baadhi ya nchi za kiafrika
ambazo zinakuwa ikiwemo maswala kama ukuwaji wa uchumi, uekezaji na
biashara pamoja na kukuza taasisi za kidemokrasia na kuendelea kukuza
viongozi wa kizazi kijacho Afrika,'' ilinukuu taarifa kutoka ikulu ya
White House.
Soma zaidi
No comments:
Post a Comment