EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, July 10, 2014

HOMA YA BONDE LA OFA WAIBUKA MKOANI SIMIYU SERIKALI YATOA TAHADHALI KWA WAKAZI WA MKOA HUO


Paschal Mabiti


Serikali mkoani Simiyu imewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa, ambao umeonyesha dalili za kurejea mkoani hapa.

Ugonjwa huo hatari ambao huwashambuliwa wanyama pori na mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda, unaelezwa kurejea tena mkoani Simiyu baada ya baadhi ya mifugo kugundulika kushambuliwa.

Mkuu wa Mkoa huo, Paschal Mabiti, alitoa tahadhari hiyo katika kikao cha wadau wa afya ya msingi cha mkoani hapa.

Alisema tayari viashiria vya ugonjwa huo, ambao ni hatari kuliko homa ya Dengue, vimeonekana mkoani hapa.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa mapema katika vituo vya afya, ikiwa watahofia kuwapo kwa dalili za ugonjwa huo.

Pia aliwataka wafugaji wote, hususan wanaoishi kandokando ya mbuga za wanyama pamoja na wale wanaotumia nyama kutoa taarifa juu ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Homa hiyo, ambayo ilileta maafa mwaka 2006 hadi 2008, inalelezwa kuwa ni hatari, hasa kwa wafugaji wanaoishi kando ya hifadhi na pembezoni.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment