EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, June 29, 2014

BRAZIL LEO KUTAWALIWA NA AFRIKA NI NIGERIA NA ALGERIA 16 BORA

LEO Usiku huko Brazil, Timu za Afrika, Nigeria na Algeria, zipo dimbani kwenye Mechi za Raundi ya Pili ya Mtoano ya Kombe la Dunia.

Nigeria ndio itakuwa ya kwanza kutinga Uwanja wa Nacional Mjini Brasilia kucheza na France na kufuatia Algeria ambao watacheza Uwanja wa Beira-Rio huko Porto Alegre dhidi ya Germany.
PATA TATHMINI FUPI:
Nigeria v France
NIGERIA-AHMED-MUSSABaada kuiendesha puta Argentina kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi lao na kushindwa kiume kwa Bao 3-2, Nigeria sasa wanaivaa France wakisaka tiketi ya kucheza Robo Fainali.
Kocha wa France, Didier Deschamps, anatarajiwa kuwarudisha Wachezaji kadhaa Kikosini baada ya kuwapumzisha kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi dhidi ya Ecuador.
Wachezaji hao ni pamoja na Evra, Cabaye na Valbuena.
Nguvu ya France ipo hasa kwenye Kiungo ambapo Cabaye, Matuidi na Pogba hushirikiana vizuri kumchezesha Straika wao Karim Benzema.
Nigeria nguvu yao kubwa ipo kwenye mashambulizi yao ya kasi huku Mastraika wao Ahmed Musa na Peter Odemwingie wakiwa wapesi kuziona nyavu.
VIKOSI VINATARAJIWA:
France: Lloris; Debuchy, Koscienly, Varane, Evra; Sissoko, Valbuena, Matuidi, Pogba; Griezmann, Benzema.
Nigeria: Enyeama; Ambrose, Oshaniwa, Omeruo, Yobo; Mikel, Onazi, Emenike, Babatunde; Odemwingie, Musa.
REFA: Mark W. Geiger [USA]
Algeria v Germany
Germany wametinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada ya kushinda Mechi 2 na Sare moja kwenye Kundi lao.
Germany waliwatwanga Portugal 4-0 na USA kuitungua 1-0 na kutoka Sare 2-2 na Ghana.ALGERIA-SLIMANI
Straika wa Bayern Munich, Thomas Muller, ameifungia Germany Bao 4 ikiwemo Hetitriki walipocheza na Portugal.
Algeria wao kwenye Kundi lao walianza kwa kufungwa 2-1 na Belgium, kisha kuitwanga South Korea 4-2 na kutoka Sare 1-1 na Russia na kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Algeria, chini ya Kocha Vahid Halilhodzic, ni Timu imara huku Islam Slimani akiwa hatari katika ufungaji.
Pia Algeria wana rekodi nzuri dhidi ya Germany kwani waliwahi kuwafunga 2-1 kwenye Mechi yao ya ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia huko Spain Mwaka 1982.

VIKOSI VINATARAJIWA:
Germany: Manuel Neuer; Benedikt Höwedes, Mats Hummels, Per Mertesacker, Jerome Boateng; Sami Khedira, Philipp Lahm, Toni Kroos; Mario Götze, Mesut Özil, Thomas Müller
Algeria: Mbolhi; Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam; Mostefa, Taider; Feghouli, Brahimi, Soudani; Slimani
REFA: Sandro Ricci [Brazil] 
KOMBE LA DUNIA
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
**Saa za Bongo

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil 1 Chile 1, Penati 3-2
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia 2 Uruguay 0
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador
ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Mshindi 53 v Mshindi 54 [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

2300
Brazil v Colombia [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza

JUMAMOSI, JULAI 5, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Mshindi 55 v Mshindi 56 [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia

2300
Mshindi 51 v Mshindi 52 [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador

NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte

JUMATANO, JULAI 9, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 59 Mshindi 60 [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo

MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia

FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

No comments:

Post a Comment