EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 13, 2014

MAAFISA WATENDAJI WA KATA WAPEWA ONYO KALI,MKUU WAWILAYA MTWARA ASEMA HAKUNA CHEO WALA KUFAHAMIKA KAMATAKAMATA IANZE MARA MOJA KWA WANAOWEKA MIFUGO KATIKATI YA MJI.


MKUU WA WILAYA YA MTWARA MH: WILLMAN NDILE KWA MBALI AKIZUNGUMZA NA WATENDAJI WA KATA WAKATI WA KIKAO.
NA KASSIM NGUMBI ……..Mtwara
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara MH: Willman Kapenjama Ndile Katika kikao kilichofanyika jana ndani ya ukumbi wa boma kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa mtwara ambacho kilihusisha maafisa watendaji wa mitaa toka manispaa ya Mtwara Mikindani,wakuu wa idara wa manispaa akiwemo Daktari wa manispaa, Mwanasheria wa Manispaa Afisa Afya na Afisa Utumishi pamoja na watu wanaotoka sektwa za ulinzi na usalama kwa maana ya ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa na ofisi ya jeshi la magereza la mkoa na mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani na kuchukua takribani masaa mawili na nusu kuanzi saa nane za mchana mpaka saa kumi alaasiri.
BAADHI YA WAJUMBE WAKIWA KIKAONI
Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuzungumzia mambo yapatayo matatu ambapo la kwanza lilikuwa ni swala nyeti la usafi wa mji,lapili ni swala la uwepo wa mifugo kupitiliza katikati ya mji, na swala la tatu ni swala la upigaji muziki kupita kiasi katika nyakati za usiku maeneo ya baa zilizopo katikati ya makazi ya watu.
Awali katika maelezo yake kabla ya kuanza kuzungumzia haya mh dc  alieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na tamko lake alilokalitoa wiki mbili zilizopita la kuwataka wazazi wote ambao bado hawajawapeleka watoto wao ambao wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zao na kutoa agizo la kwamba wasipofanya hivyo basi watachukuliwa hatua kali za kisheria. Awali katika tamko lake hilo Ndile alitoa siku saba kwa wazazi kutekeleza agizo hilo na wakati tamko hilo likitoka uwiano wa watoto kwenda mashuleni kwa upande wa halmashauri ya mtwara vijijini ambayo ipo ndani ya wilaya yake ni watoto watatu tu katiya kumi ndio waliokua wamepelekwa shule huku saba wakisalia nyumbani bila sababu maalum na kwa upande wa manispaa ya mtwara mikindani uwiano ulikuwa ni watoto saba kati ya kumi ndio waliojiunga na kidato cha kwanza huku idadi kamili ya watoto waliotakiwa kuanza kidato cha kwanza ikiwa ni 1090. Lakini mpaka kufikia jan adc ndile alisema kuwa watoto 1083 tayari wamekwishaanza masomo na watoto saba tu ndio wamesalia huku akiahidi kuwa baada ya wiki moja nao watakua wamekwenda shuleni kwa muhula mpya wa masomo ya sekondari katika hili alitoa pongezi kwa maafisa watendaji wa kata,mitaa na viongozi wa serikali za vijiji pamoja na vyombo vya habari ambao wao walikuwa ni wadau wakubwa katika kuhamasisha na kuhakikisha hili swala linafanikiwa.

MAMBO MATATU YA KIKAO CHA JANA

1.       SWALA LA KUZAGAA KWA MIFUGO KATIKATI YA MJI……kuhusu hili mkuu wa wilaya alinukuu baadhi ya taarifa alizopelekewa juu ya kuwepo kwa hali ya kuzagaa kwa ng’ombe, mbwa na nguruwe katika maeneo mengi ya mitaa ya katikati ya mji ambapo mifugo hii inasababisha kero kubw kwa wakazi wa maeneo husika , akianza na swala la ng’ombbe MH: NDILE alisema kuwa yeye mwenyewe amekwishawahi kushuhudia makundi makubwa ya ng’ombe wakikatiza katikatio ya mji na kutaka kusababisha ajali lakini pia uwepo wa mifugo ya aina hiyo ndani ya mji ni uchafu hivyo amewataka watendaji wa mitaa kuhakikisha wanakamata mifugo nhiyo bila kujali nani mmiliki kwa kuzingatia sheria na kuwatoza faini ya shili elfu sitini.
Lakini katika maeneo haya ya mifugo mkuu wa wilaya alizungumzia pia suala la nguruwe na mbwa akasema kuwa nguruwe wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi wengi kwa kutoa harufu mbaya katika makzi wanayoishi na kusababisha uharibifu wa hari ya hewa lakini pia mpaka sas amekwishapokea kesi za watu waliong’atwa na mbwa zipatzo ishirini hivyo hili nalo limekuwa kero na akataka watendaji kuhakikisha wanafuata sheria ambayo inataka kila mfugaji ndani ya mji asifuge zaisdi wa wanyama watatu na akasema kuwa iwapo wanyama kwama mbwa wakiwa wengi na ni kero basi watendaji wanao uwezo wa kuandika muhtasari wa kuamuru kuuawa kwa mbwa hao.
2.       MUZIKI KUPITILIZA…….PIA katika maelezo yake alisema kuwa sheria hiyo inazuia tabia ya kupiga muziki kupitiliza nyakati za usiku hasa katika mabaa na mikesha ya sherehe mbalimbali kwani swala hilo pia ni kero kwa wananchi wengine na kwamba mtu atakayehitaji kufanya biashara ya muziki basi ahakikishe anajenga ukumbi wenye sound proof na hili pia mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo kwa watendaji hao wa kata kulisimamia huku akihusisha na nyumba za ibada ambazo zimekuwa zikipiga vyombo vyao kwa sauti za juu sana bila kuzingatia eneo kanisa au msikiti ilipo.
3.       USAFI WA MAZINGIRA…….mwisho amewataka watendaji hao kutumia sheria walizokabidhiwa jana kwa kuhakikisha kila eneo ndani ya mji na wilaya mzima linakua safi kwa kufyeka majani na kusafisha mitaro ili kuufanya mji wa Mtwara uwe na mazingira mazuri. Watendsaji wote ambao walihudhulia jana katika kikao hicho wamekabidhiwa nakala za sheria ambapo wamepewa wiki moja kuzipitia na baada ya hapo atatangaza amri ya utekerezaji way ale yote waliyokubaliana kupitia kikao hicho.

No comments:

Post a Comment