Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda.
DPP aliwasilisha pingamizi la awali dhidi ya Sheikh Ponda mbele ya Jaji Augustino Mwarija akidai maombi yake hayana mashiko ya kisheria.
Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernad Kongola na utetezi ni Mawakili Juma Nassoro na Obeid Hamidu.
Katika pingamzi hilo, DPP anadai kuwa maombi ya Sheikh Ponda hayaruhusiwi kusikilizwa mahakamani hapo chini ya kifungu cha 372 kidogo cha 2 cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kifungu hicho kinaeleza kwamba mtu hataruhusiwa kuwasilisha maombi yoyote ya marejeo ambayo yanatokana na maamuzi au amri ya mahakama ya chini ambayo hayakumaliza kesi.
Akijibu hoja za DPP, wakili wa utetezi Juma alidai kuwa, maombi hayo yana mashiko ya kisheria na kwamba mshtakiwa ana haki ya kusikilizwa na mahakama hiyo.
Katika kesi ya msingi, Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka ya kukaidi amri halali, kuharibu imani za dini, kushawishi na kutenda kosa.
Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment