EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, March 12, 2014

ASILIMIA 35 YA WASICHANA WA UMRI WA MIAKA 10 MPAKA 18 MKOANI MTWARA WANA WATOTO NA WENGI WAO HAWANA MSAADA WA MAISHA HUKU WAKIWA HAWANA ELIMU.


Mkurugenzi Mtendaji wa KIWOHEDE. BI: JUSTA MWAITUKA
NA KASSIM NGUMBI:….Mtwara 
TAASISI isiyo ya kiserikali inayojihusisha na usimamizi wa kuwakomboa wsichana walio katika mazingira magumu hasa wale wa kuanzia miaka 10 mpaka 18 na ambao wameathiriwa na tatizo la ngono za utotoni KIWOHEDE (Kiota Women Health And Development Organisation) imezindua tawi la taasisi yake mkoani mtwara ambalo ofisi zao zitakuwa mitaa ya ligula B kata ya chuno karibu na baa ya amigio kwa lengo la kukusanya na kuwasaidia wasichana walioko katika mazingira hatarishi hasa vishawishi vya kujiingiza katika biashara za ngono na kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi. Akizungumza mapema leo asubuhi  Mkurugenzi wa kampuni hiyo BI:JUSTA MWAITUKA amesema kwamba wao kama taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa uzoefu sasa kupitia matawi yao zaidi ya 16 wameona umuhimu wa kuwa na kituo mtwara kwa kutokana na takwimu walizozipata wakati wa uandaaji wa ukusanyaji wa maoni ya rasimu ya katiba uliofanywa na vijana wao katika mkoa wa mtwara na kubaini kuwa kumekuwa na hali ya muonekano wa awali wa vijana na wasichana kuanza kujiingiza katika masuala hatarishi hususani biashara ya ngono. 
 Aidha amesema kuwa swala linguine lililowavuta kufanya kazi mtwara ni kutokana na kugundulika kwa nishati asilia za mafuta na gesi kwani mara nyingi mahali penye miradi hiyo huwa panatawaliwa na vitendo ambavyo si vizuri vikiwemo vya ngono ambayo si salama na inayohusisha mabinti wa umri mdogo. BI: JUSTA wakati akizungumza na SWACOTZ FORUM kupitia kituo cha redio cha PRIDE FM alisema kwa sasa wao wamelenga kudili na wasichana 750 kwa kila awamu ya utekerezaji yaani mwaka mmoja katika mradi wao ambao utakuwa ndani ya kata tano za manispaa ya Mtwara Mikindani na tayari wamekwishaanza shughuli ya ukusanyaji wamakundi hayo ya wasichana kwa kushirikiana na uongozi wa maeneo  husika na katika maelezo yake alisema kuwa katika semina ya awali iliyohusisha wasichana 102 toka katika kata hizo walibaini kuwepo kwa wasichana wawili tu ambao ndio bado wanasoma na wawili ndiowaliomaliza kidato cha nne huku wasichana zaidi ya 40 wakiwa tayari na watoto wakati walosalia wakiwa hawana elimu kwani walishindwa kumaliza shule kutokana na tatizo la mimba na mengineyo idadi ambayo inapelekea kufikia zaidi ya asilimia 35 ya wasichana kuwa wako katika mazingira magumu na kusema kuwa hii ni changamoto kwa mtwara kwani idadi ni kubwa na wanapaswa kuchukua hatua na kushirikiana na KIWOHEDE katika harakati za kukomesha mambo haya ,lakini mradi huu umelenga kusaidia wasichana 1500 katika awamu mbili za mradi kwa muda wa miaka miwili na katika utekerezaji wake tayari wameandaa namna ya kuwasaidia wasichana hao ikiwemo kuwapatia taaluma kwa kuwapeleka katika vyuo mbalimbali kama vile VETA na wengine watakua wakifundishwa na wkufunzi katika kituo hicho cha KIWOHEDE mtwara kwa taaluma ya vitu mbalimbali lakini pia akasema kuwa kwa wale ambao watakua wamefaidika na mradi huu mpaka mwisho basi watawezeshwa vifaa vya kiutendaji kutokana na taaluma yake hivyo amewaomba wasichana wa mtwara kupitia kata husika za mradi kuacha fikra mgando na badala yake wajihusishe na KIWOHEDE ili waweze kupewa uwezo na ufahamu wa namna ya kujikomboa katika maisha na kuepukana na hatari iliyopo mbele yao juu ya tatizo la biashara za ngono inayotokana na wengi kutokuwa na mwelekeo wa maisha.
 

No comments:

Post a Comment