
Wabunge
wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida
Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu)
wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye
Uwanja wa Soweto jana.
Mkuu
wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jana kwamba
pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu wapatao 60 kutokana na
vurugu zilizozuka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo
waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi,
Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea
kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.
Mbali ya viongozi...
NAPE , GODBLESS LEMA NA MBOWE WATAKIWA KUPELEKA ASHAHIDI WAO POLISI, VINGINEVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

Jeshi la Polisi limetishia kuwakamata Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na limesema
litamhoji Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wanasiasa hao
kudai kufahamu watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha
jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja aliwataka
wanasiasa hao kuwasilisha ushahidi wa kile wanachofahamu kuhusu
kulipuliwa kwa bomu hilo.
Juzi, Mbowe akiwa na Lema, alisema wana ushahidi
wa picha za video zikiwahusisha polisi na kulipuliwa kwa bomu...
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WABUNGE 4 WA CHADEMA KWA KUSABABISHA VURUGU ARUSHA

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA
na watu wengine huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili na watu
wengine.Jeshi la Polisi limesema limewatua nguvuni watu hao kwa
makosa ya kuhutubia mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu
waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la
Soweto jijini humo mwishoni mwa wiki.Makosa mengine ni wanayotuhumiwa
kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.Amesema
wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.Kamanda wa
Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amewataja Wabunge wanaoshikiliwa
ni pamoja na Tundu Lissu na Mustapha...
SABABU ZA JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU YA MABOMU JIJINI ARUSHA MUDA HUU

Jeshi
la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na
maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu
kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea
kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu
upelelezi.
Kamanda
Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama
hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli
hiyo lakini...
BREAKING NEWS: ARUSHA KWACHAFUKA TENA.....MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WANANCHI

Hali kutoka mkoani si nzuri...mabomu ya machozi yanapigwa kuwatawanya
wananchi waliojitokeza kuiaga miili ya wananchi waliofariki katika
mlipuko wa bomu...
Hivi sasa polisi wanapiga mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa
CHADEMA
waliofurika katika uwanja wa Soweto Mjini Arusha ulipotokea mlipuko wa
bomu Jumamosi kuomboleza ambapo polisi inasema mkusanyiko huo si halali
Taarifa toka mkoani humo zinadai kuwa gari
la mh. Lissu liteketezwa vibaya kwa bom...
MBUNGE ATAKA KISWAHILI KITUMIKA HADI VYUO VIKUU

MBUNGE wa Karagwe, Gosbert Blandes
(CCM), amehoji lini serikali itapitisha Kiswahili kitumike kuanzia Shule
za Msingi hadi Vyuo Vikuu. Aidha, alisema mwaka 2004, Umoja wa Afrika
ulipitisha Kiswahili kiwe ni lugha ambayo itatumika katika mikutano na
shughuli mbalimbali.
“Je, serikali imejiandaa vipi kupeleka wakalimani wa kutosha kutoka Tanzania ili waweze kujipatia ajira?” alihoji.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala alisema jitihada
zinafanywa na taasisi hizo za kukuza Kiswahili mojawapo kuandika vitabu
vingi vya kufundishia na kuongeza wataalamu.
“Nasema wazo hilo tumelipokea...
MOTO MKALI WATIKISA MAENEO YA KARIAKOO JIJINI DAR

Hali ikiwa tete.
Moto ukiunguza paa la baa hiyo.
Shock ya umeme ikitokea karibu na jengo hilo.
Watu waliojaa kushuhudia tukio hilo.
Moto
mkubwa umezuka jijini Dar es Salaam karibu kabisa na Soko Kuu la
Kariakoo leo asubuhi na kuteketeza baa moja. Chanzo cha moto huo
inadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme iliyotokea jirani na baa hiy...
No comments:
Post a Comment