Hivi ndivyo
ilivyokuwa ajali hiyo iliyohusisha Lori na Coaster katika eneo la Mbalizi
Baadhi ya
wananchi wakishuhudia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 10:45 leo jioni
katika eneo la Mlima Iwambi kuelekea Mbalizi
Baadhi ya
askari polisi wakilinda mali zilizokuwemo katika Lori, hata hivyo askari hao
walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya watu waliotaka kupora bidhaa
hizo.
Mmoja wa
majeruhi wa ajali akiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya akisubiri kupatiwa
matibabu.
Wauguzi wa
huduma ya haraka katika hospitali ya Rufaa Mbeya wakimpatia huduma mmoja wa
majeruhi wa
ajali hiyo.(Picha kwa hisani ya Charles Abraham wa Malafyale Blog)
WIMBI la
ajali katika miezi ya Disemba na Januari nchini limeendelea baada ya ajali
nyingine kutokea mkoani Mbeya leo jioni majira ya saa 10:45 katika mtelemko wa Mbalizi na kusababisha vifo vya
watu wawili na kujeruhi wengine 23.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba magari mawili moja aina ya Coaster na Lori
la mizigo yalikuwa yakielekea njia ya Tunduma kutokea Jijini Mbeya ambapo lori
hilo linadaiwa kuharibika mfumo wa breki likiwa mtelemkoni.
Lori hilo la
mizigo aina ya SCANIA lenye namba za usajili T 101 CRL na trela lenye namba za
usajili T 859 BZW ambalo lilibeba bidhaa mbalimbali za madukani liliigonga
Coaster yenye namba za usajili T 910 BFB na kusababisha magari hayo kupinduka.
source: mbeya yetu
No comments:
Post a Comment