IKIWA
Imebaki Miezi Mitatu Kabla Ya Kumalizika Kwa Mkataba Wa Kocha Wa Simba, Zdravko
Logarusic, Mwenyekiti Wa Kamati Ya Usajili Ya Klabu Hiyo, Zacharia Hans Poppe Amesema
Hatma Ya Kocha Huyo Iko Mikononi Mwa Kamati Yao Ya Ufundi.
Logarusic, Raia Wa Croatia Mwenye Umri Wa Miaka 51, Ana Mkataba Wa Miezi Sita
Kuinoa Simba Aliousaini Mbele Ya Poppe Mjini Hapa Mchana Wa Desemba 2 Mwaka
Jana Kabla Ya Kuanza Rasmi Kazi Ya Kukifundisha Kikosi Hicho Cha Msimbazi Akirithi
Mikoba Ya Mtangulizi Wake, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibadeni' Aliyetimuliwa
Mara Tu Baada Ya Mzunguko Wa Kwanza Wa Ligi Kuu Ya Vodacom Tanzania Bara Msimu
Huu.
Aidha, Katika Mkataba Huo, Kuna Kipengele Ambacho Kinatamka Kwamba Kocha Huyo
Atapewa Mkataba Mrefu Na Mnono Endapo Timu Ya Simba Chini Yake Itafanya Vizuri
Msimu Huu.
Akizungumza Mjini Hapa Leo Mchana, Poppe Amesema Kamati Ya Ufundi Ya
Simba Ndiyo Itakayoamua Hatma Ya Kocha Huyo Baada Ya Kufanya Tathimini Ya Kazi
Yake. Kamati Hiyo Inaongozwa Na Mwenyekiti Damian Manembe Na Makamu Wake, Ibrahim
Masoud 'Maestro'.
"Kamati Yangu Imekamilisha Usajili Wa Wachezaji Waliohitajika Msimu Huu,
Natambua Makubaliano Yetu Na Kocha Huyo (Logarusic) Lakini Kamati Yangu Haina
Mamlaka Ya Kumchukulia Hatua, Kamati Inayohusika Na Masuala Ya Ufundi Ndiyo Itaangalia
Kazi Yake Kabla Ya Kuamua Kumpa Mkataba Mpya Au Kuachana Naye," Amesema Poppe.
Logarusic Aliikuta Simba Ikiwa Nafasi Ya Nne Katika Msimamo Wa Ligi Kuu Ya Vodacom
Ikiizidiwa Pointi Nne Na Wapinhzani Wao Wa Jadi, Yanga Waliokuwa Vinara Yanga Huku
Ikizidiwa Pointi Tatu Na Mbeya City Na Azam FC Walikokuwa Wakikamata Nafasi Za
Pili Na Tatu.
Sasa Timu Hiyo Ambayo Keshokutwa Itashuka Ugenini Kwenye Uwanja Wa Kumbukumbu Ya
Sokoine Kuvaana Na Wababe Mbeya City Iko Nafasi Ya Nne Ikiwa Na Pointi 31 Baada
Ya Kushikwa Kwa Sare Ya Bao Moja Na Mabingwa Wa Tanzania Bara 1999 Na 2000, Mtibwa
Sugar Kabla Ya Kupata Kipigo Kisichotarajiwa Cha Bao 1-0 Kutoka Kwa Mgambo
Shooting Katika Mechi Mbili Zilizopita.
Simba Sasa Inazidiwa Pointi Tano Na Vinara Azam FC, Nne Dhidi Ya Yanga Na Tatu
Dhidi Ya Wapinzani Wao Wa Kesho Mbeya City Huku Ikiwa Imecheza Mechi Moja Zaidi
Ya Azam Na Yanga.
Ukali Wa Loga Akiwa Mazozeni Na Hata Wakati Wa Mechi, Kunaonekana Wazi Kuwa
Tatizo Kati Ya Wa Wachezaji Wa Simba Na Kocha Huyo Wa Zamani Wa Mabingwa Wa Kenya,
Gor Mahia. |
|
No comments:
Post a Comment