EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, February 14, 2014

huku ndiko iliko azam fc

Katibu Wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ Ameiambia Swacotz Mchana Jana Kutoka Beira Kwamba Timu Imefikia Katika Hoteli Ya Rainbow Na Mechi Itachezwa Jumapili Saa 8:00 Mchana Kwa Saa Za Msumbiji Na Saa 10:00 Jioni Kwa Saa Za Afrika Mashariki.
Father Amesema Mchezo Huo Utaonyeshwa Moja Kwa Moja Na Televisheni Ya Azam TV.
“Lakini Mvua Kubwa Inanyesha Huku, Inanyesha Kutwa Nzima, Ila Maandalizi Ni Mazuri Na Tumekuja Na Viatu Vya Kuchezea Kwenye Mvua, Hivyo Tupo Kamili,”Alisema Father.
Azam FC Iliyoanza Kwa Ushindi Mwembamba Wa 1-0 Jumapili Uwanja Wa Azam Complex Jumapili, Iliondoka Jana Asubuhi Dar Es Salaam Kwa Ndege Ya Fast Jet Hadi Johannesburg, Afrika Kusini Ambako Waliunganisha Ndege Ya Shirika La Msumbiji Kwenda Beira.


Azam Imeondoka Na Wachezaji 21 Ambao Ni Makipa; Mwadini Ali, Aishi Manula Na Jackson Wandwi, Mabeki Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, David Mwantika, Viungo Ibrahim Mwaipopo, Kipre Balou, Jabir Aziz, Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha Na Washambuliaji John Bocco, Kipre Tchetche, Brian Umony, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba Na Ismael Kone.



No comments:

Post a Comment