EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, December 5, 2013

ROBBEN AUMIA GOTI.


KIUNGO mahiri wa klabu ya Bayern Munich, Arjen Robben anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda baada ya kuumia goti katika mchezo wa jana.
 
 Robben mwenye umri wa miaka 29 aliifungia Bayern bao katika dakika ya nne kwenye mchezo wa Kombe la Ujerumani dhidi ya Augsburg lakini alitolewa kwa machela dakika 12 baadae kwa kugongana na golikipa wa timu pinzani Marwin Hitz.
 
 Madaktari wa timu hiyo wamedai kuwa baada ya kufanyiwa vipimo zaidi ndipo wanatajua ni muda gani nyota huyo atakaa nje ya uwanja. Robben amekuwa katika kiango cha juu katika mechi za hivi karibuni akiwa amefunga bao katika mechi zilizopita.

No comments:

Post a Comment