NA SHARIFA
MMASI
KOCHA mkuu
wa maafande wa Polisi Morogoro Mohamed Richard Adof, amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi
kabambe, hawatashuka daraja tena
Kocha huyo
alisema kikosi chake kinaendelea na mzoezi makali ambayo yataleta mafanikio
katika timu ikiwa ni pamoja na kuondoa
sura mbaya ya timu hiyo ya kupanda na kushuka daraja kila msimu.
Adol
alisema kila timu inafanya maandalizi ya nguvu kwa ajili ya kuleta ushindani
kwenye Ligi, kwa kutambua hilo wanajitahidi kujipanga vizuri ili kuja kukabilia
na changamoto za Ligi hiyo.
Timu ya
Polisi ilishuka daraja msimu wa mwaka 2012/13 pamoja na timu za African Lyon na
Toto African ya Mwanza kabla ya kufanikiwa kupanda tena msimu huu.

No comments:
Post a Comment