Iringa. Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema tatizo la umaskini
linalowakabili Watanzania, linatokana na viongozi walioko madaraka
kutokuwa waadilifu.
Alisema
Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi ambazo kama
zikisimamiwa vyema taifa haliwezi kuwa na watu maskini kama ilivyo hivi
sasa.
Dk
Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mikutano ya
kampeni iliyofanyika katika Vijiji vya Igula katika Kata ya Luwota na
Magulilwa mkoani Iringa.
“Nchi
hii siyo maskini, imejaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa
ipaswavyo, taifa lisingekuwa na umaskini kama ilivyo sasa,” alisema Dk
Slaa na kuongeza:
“Leo hii viongozi wa CCM wamekosa uadilifu ndiyo maana magogo kutoka katika misitu yetu yanaibiwa na kupelekwa nje ya nchi.
Dk
Slaa alisema hayo yanatokana taifa kuongozwa na watu wasio waadilifu,
huku Amiri Jeshi Mkuu ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya
Kikwete akishindwa kukabiliana na hali hiyo. Katika mikutano hiyo, Dk
Slaa aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua mbunge wao ili kuongeza idadi
ya wabunge wake
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka wananchi wa Jimbo la
Kalenga mkoani hapa kutambua kuwa chama hicho kipo kwa lengo la
kuwatetea wananchi bila kujali itikadi za vyama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Ifunda, Dk. Slaa alilitaka jeshi la Polisi kutenda haki kwa
vyama vyote kutokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wafuasi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo ya wapinzani pale
wanaposhambuliwa.
Alisema Jeshi la Polisi lisitumie kauli hiyo kuwanyanyasa wapinzani.
Aliwata wananchi wa Ifunda kutambua mbunge wanayemuhitaji awe na vigezo vya kujenga hoja za kuwatetea na kuwaletea maendeleo.
Wakati huo huo, Chifu wa kabila la
Wahehe, Abdu Sapi Mkwawa, amevitaka vyama vilivyosimamisha wagombea
Kalenga kuendesha kampeni zao kwa amani na utulivu, na akatoa baraka
zake kwa mgombea wa CHADEMA na kumtakia ushindi katika Jimbo la Kalenga.
No comments:
Post a Comment