Sneijder, Mchezaji wa Kimataifa wa
Holland, alikuwemo kwenye Kikosi cha Inter Milan Mwaka 2010 chini ya
Jose Mourinho kilichotwaa Trebo, ikiwemo UCL.
Sneijder anaamini uzoefu wake chini ya Mourinho utaisaidia Galatasaray kuibwaga Chelsea.
Mchezaji mwingine wa Galatasaray aliewahi kuwa na Jose Mourinho ni Didier Drogba
ambae
alinunuliwa na Mourinho Mwaka 2004 kutoka Marseille na kukaa Klabu hiyo
hadi Mwaka 2012 ambako kwenye Mechi yake ya mwisho alifunga Penati ya
mwisho ya Mikwaju ya Penati 5 walipoibwaga Bayern Munich kwenye Fainali
ya UCL na kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mjini Munich.
Sneijder amedai yeye na Drogba
watamsaidia Kocha Roberto Mancini, aliewahi kuwa Manchester City,
kuandaa Timu kwa ajili ya Mechi na Chelsea.
Amesema: “Mourinho anatujua vizuri na
hilo ni udhaifu kwetu lakini hilo pia linatusaidia sisi kwani tunamjua
Mourinho vizuri sana, pengine tunamjua vyema zaidi kupita Wachezaji wa
Chelsea wanavyomjua!”
Aliongeza: “Chelsea ni Kikosi bora, kila
Mtu lazima akubali, lakini tukionyesha ari ile ile tuliyowatoa
Juventus, tunaweza kupata matokeo mengine makubwa!”
Nae Selcuk Inan, Kiungo wa Galatasaray,
vile vile anaamini Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi
inatisha kwa Timu ngeni hasa toka kwa Mashabiki wao wenye vimbwanga
kupindukia.
Amesema: “Jinsi Mashabiki wanavyotushangilia ni kitu kikubwa. Wao ni kama Mchezaji wetu wa 12!”
No comments:
Post a Comment