Enzo Zidane, mwenye Miaka 18, alizaliwa
France lakini akachukua Uraia wa Spain Mwaka 2006 na Mwaka 2009 aliitwa
kuichezea Spain U-15.
Shirikisho la Soka la France, FFF,
limethibitisha kuwa Kijana huyo atajiunga Kambi ya Mazoezi ya France
U-19 huko Clairefontaine Wiki ijayo.
Willy Sagnola amesema: “Mchezaji
ameamua kuvaa Jezi ya Bluu kwa sasa. Baadae anaweza kubadilika lakini
nia yake ni kuichezea France.”
Enzo Zidane anaweza kuamua kuzichezea
Nchi za Spain, France na hata Algeria wanakotoka Babu zake atakapoamua
kwani Mechi za Kirafiki, kwa mujibu wa Kanuni za FIFA, hazimfungi
Mchezaji kucheza Mashindano rasmi Nchi hiyo hiyo aliyovalia Jezi.
Mtoto huyo wa Zinedine Zidane, ambae
sasa ni Kocha Msaidizi wa Real Madrid chini ya Carlo Ancelotti,
alijiunga na Timu za Vijana za Real Madrid tangu 2004.
Enzo Zidane ni mmoja wa Watoto wa
Kiume wanne wa Zidane na Mama yao Veronique Fernández wengine wakiwa ni
Luca, Theo, na Elyaz, na wote huchezea Timu za Vijana za Real Madrid za
Marika tofauti.
No comments:
Post a Comment