BAADA Klabu zote za England, Arsenal,
Manchester City na Manchester United, zote kupigwa Bao 2-0 kwenye Mechi
za Kwanza za UEFA CHAMPIONZ LIGI, Raundi ya Mtoano Timu 16, Usiku huu
Chelsea ‘waling’ara’ baada kutoka Sare 1-1 huko Türk Telekom Arena Ali
Sami Yen Spor Kompleksi, Jijini Istanbul, Uturuki, walipocheza na
Galatasaray Spor Kulübü.
Huko
Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi, Jijini Istanbul,
Uturuki, Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 9 la Fernando
Torres kufuatia ushirikiano mzuri wa Andre Schurrle aliempasia Fulbeki
aliepanda juu, Cezar Azpilicueta, ambae huku Kipa Fernando Muslera akiwa
ametoka Golini, alimpasia, Fernando Torres aliemalizia vizuri.
Bao hilo, ambalo lilidumu hadi Haftaimu, pia lilichangiwa na makosa ya Beki wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue.
Katika Dakika ya 54, Galatasaray
walisawazisha baada ya Kona ya Wesley Sneijder kukoswa na Jerry Terry na
Aurelien Chedjou kuunganisha wavuni.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, ambae hakuwika, alibadilishwa katika Dakika 10 za mwisho na kuingizwa Umut Bulut.
VIKOSI:
Galatasaray: Muslera, Alex, Balta, Chedjou, Eboue, Sneijder, Inan, Felipe Melo, Hajrovic, Drogba, Burak Yilmaz
Akiba: Ceylan, Gulselam, Bulut, Kaya, Kurtulus, Colak, Sarioglu.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Cahill, Terry, Ivanovic, Hazard, Lampard, Ramires, Willian, Schurrle, Torres
Akiba: Schwarzer, Cole, Oscar, Mikel, Ba, Eto'o, Kalas.
Refa: Carlos Velasco Carballo (Spain)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC [2-0]
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan [1-0]
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City [2-0]
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen [4-0]
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]
No comments:
Post a Comment