EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, December 5, 2013

MAROTTA "POGBA ATANYAKUWA TUZO YA BALLON D'OR SIKU ZA MBELE "


MKURUGENZI mkuu wa klabu ya Juventus, Giuseppe Marotta anaamini kuwa mshambuliaji nyota wa timu hiyo Paul Pogba ana nafasi ya kushinda taji la Ballon d’Or siku za mbele.
 Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 20 alishinda tuzo Golden Boy mapema wiki hii mbele ya wachezaji wengine waliokuwa wakigombea tuzo hiyo kama Romelu Lukaku na Julian Draxler.
 Marotta amesema hana shaka kuwa Pogba ataweza kunyakuwa tuzo hiyo kubwa kabisa kwa wachezaji katika siku za mbele na ni mategemeo yake atafikia mafanikio hayo wakiwa naye hapo Juventus.
 Pogba alijiunga na Juventus akitokea Manchester United katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2012 na toka kipindi hicho ameshacheza mechi 50 kwa mabingwa hao wa Serie A.

No comments:

Post a Comment