EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 10, 2013

WATOTO 946 WAPOTEZA MAISHA MKOANI9 MARA



WATOTO 946 walio chini ya umri wa miaka mitano mkoani Mara, wamepoteza maisha kutokana na malaria kati ya Januari na Desemba mwaka 2012.


Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa, amesema hayo hivi karibuni wakati akifungua kikao cha uhamasishaji wa kampeni ya kunyunyizia dawa ya kuua mbu wanaoeneza malaria.





Tuppa amesema malaria ni ugonjwa hatari unaoenendelea kupoteza maisha ya watu wengi, na kwamba mtu mmoja hupoteza maisha kila dakika, ambapo kitaifa wagonjwa 60,000 hufariki dunia kwa mwaka kwa malaria.
Kwa mujibu wa Tuppa, takwimu zinaonesha kuwa mkoani Mara maambukizi ya malaria kwa watoto ni asilimia 25, ikilinganishwa na mikoa jirani ambayo ni Mwanza, Geita, Kagera na Simiyu.
Kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, hasa kwa Kanda ya Ziwa, serikali kupitia kitengo cha kupambana na malaria chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mfuko wa Rais wa Marekani, chini ya Shirika la Misaada la watu wa Marekani, inatekeleza mradi wa upulizaji dawa ya kuua mbu majumbani.
Mratibu wa malaria mkoani hapa, Tukae Lisso, amesema mzunguko wa tatu wa awamu ya pili, umelenga kupulizia dawa hiyo kwa kaya 24,698 kwenye wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti.

No comments:

Post a Comment