Watu zaidi ya 10,000 wameripotiwa kufariki dunia
nchini Ufilipino katika jimbo la Leyte, baada ya dhoruba ya kimbunga kikali cha
Haiyan kuikumba nchi hiyo, na kusababisha pia uharibifu mkubwa.
Mkoa wa kati wa Leyte ni miongoni mwa maeneo
yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga hicho, kilichoanzia mashariki na kuelekea hadi
magharibi mwa Ufilipino.
Barabara za mji wa Tacloban mkoani humo zimefunikwa
na maji au hazipitiki, kutokana na kuangukiwa na miti huku maiti za watu zikiwa
zimetapakaa huku na kule.
Watu wapatao laki nane walilazimishwa kuyahama makazi
yao katika tahadhari iliyochukuliwa kukabiliana na kimbunga cha Haiyan.
Sebastian Rhodes Stampa, mkuu wa timu ya Umoja wa
Mataifa ya Uratibu wa Tathmini ya Maafa aliyeko Tacloban amesema ukubwa wa
maafa kama hayo yaliyosababishwa na kimbunga cha Haiyan aliyashuhudia baada ya
Tsunami iliyotokea katika Bahari ya Hindi.
No comments:
Post a Comment