EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 10, 2013

MILA NA DESTURI ZA KIMASAI KUSAIDIA ELIMU DHIDI YA UKIMWI



Jamii za wafugaji wa Kimasai na Kimang’ati, zimetakiwa kutumia desturi na mila zao, kama nyenzo ya kupata elimu jinsi ya kujikinga na magonjwa, maambukizi ya Ukimwi, uzazi na afya bora.


Akifungua warsha ya viongozi wa kimila wa jamii za wafugaji jijini Dar es Salam, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete amesema jamii isiyo na mila imekufa, hivyo hakuna mila wala tamaduni potofu, bali zifanyiwe marekebisho kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Amesema ili kuhakikisha yote hayo yanawezekana, ni kutoa elimu kwa vijana kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mimba za utotoni.
Mama Salma amesema kwa kutumia desturi na mila hizohizo kwa majadiliano yatakayofanyika kwenye warsha hiyo, jamii hizo zinaweza kuweka mipango inayowahakikishia vijana usalama, kwa ajili ya kuendeleza mila huku zikijikinga na magonjwa.

No comments:

Post a Comment