Serikali
imetoa wito kwa halmashauri nchini, zinazohusika katika mikoa itakayokabiliwa
na njaa, kufuatilia kwa karibu utaratibu wa kupata chakula kinachotolewa kutoka
maeneo yenye ziada, na kuhakikisha kuwa kinafika mapema kwenye maeneo yao,
kabla ya wananchi wa maeneo hayo hawajaanza kulalamika.
Wito huo wa serikali umetolewa na Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Bunge la 10, katika
Mkutano wa 13 mjini Dodoma, ambaye amesema halmashauri 61 zinatarajiwa kukumbwa
na uhaba wa chakula. Ameitaja
mikoa ya halmashauri zitakazokabiliwa na uhaba huo kuwa ni Manyara, Shinyanga,
Simiyu, Arusha, Dodoma, Lindi, Tanga, Singida, Mara, Morogoro, Kilimanjaro,
Mwanza, Pwani, Mtwara, Kigoma na Tabora.Waziri
mkuu amesema serikali inaendelea na tathmini ya kina ya hali ya chakula na
lishe katika halmashauri 61, kwa lengo la kubainisha idadi ya watu wenye uhaba
wa chakula ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo Amewataka
Wakala wa Taifa na Hifadhi ya Chakula, kujipanga vizuri kuhamisha chakula
kutoka maeneo yenye ziada na kupeleka kwenye maeneo yenye hali tete ya uhaba wa
chakula.
No comments:
Post a Comment