Gavana wa jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan,
amesisitiza juu ya kupambana na makundi ya waasi jimboni humo, na kusisitiza
kuwa hatawavumilia waasi vyovyote iwavyo.
Adam Al-Faki ameongeza kuwa, idara ya kieneo ya
jimbo hilo imepanga mikakati madhubuti kwa ajili ya kulisafisha jimbo hilo
kutokana na uwepo wa makundi ya wabeba silaha.Ameitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuwaachilia
huru watuhumiwa wa ujasusi, kuwarejesha kazini baadhi ya watu waliokuwa
wamefutwa kazi, kuimarisha usalama na uthabiti na kuinua kiwango cha kujiamini
jimbo hilo.Hata hivyo amesema kuwa, makundi ya wabeba silaha
yamekuwa yakikwamisha mikakati hiyo ikiwemo kutekeleza mashambulizi dhidi
ya baadhi ya miji na mauaji ya watu wasio na hatua.
No comments:
Post a Comment