Majaji nchini Misri wamesema kiongozi wa zamani wa nchi
hiyo Hosni Mubarak pamoja na wanawe wawili, atapandishwa tena kizimbani, kwa
tuhuma za kuhodhi na kupora mali za taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mubarak na wanawe ambao
ni Alaa na Gamal wanatuhumiwa kupora kiasi cha Lira milioni 125 za nchi hiyo,
sawa na Euro milioni 13, kutoka katika ofisi ya rais.
Uchunguzi unaonesha kuwa, watuhumiwa wanne wengine
wa faili hilo, ni watu waliomsaidia Mubarak na wanawe katika uporaji wa kiasi
hicho cha fedha.Ikumbukwe kuwa, Mubarak pamoja na Waziri wa Mambo ya
Ndani wa serikali yake na watu wengine sita katika uongozi uliopita, wanatuhumiwa
kushiriki katika mauaji dhidi ya waandamanaji katika machafuko ya mwaka 2011,
yaliyopelekea kung’olewa madarakani kwa utawala wake.
No comments:
Post a Comment