MABINGWA
WATETEZI na Vinara wa La Liga, FC Barcelona, Jana Usiku wamerudi
kileleni mwa Ligi hiyo ya Spain baada ya kuinyuka Malaga Bao 3-0
Uwanjani Nou Camp.
Bao za Barca zilifungwa na Gerard Pique, Dakika ya 40, Pedro Dakika ya 55 na Sanchez Dakika ya 61.
Jumamosi, Real Madrid walitwaa uongozi
wa Ligi lakini mapema Jana ushindi kwa Atletico Madrid uliwafanya wao
wakae juu na sasa Barca wamerudi kileleni na kuiacha Atletico ishike
Nafasi ya Pili ingawa wamefungana kwa Pointi huku Real wakikamata Nafasi
ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma yao.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LA LIGA:
MSIMAMO-Timu za Juu:
|
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
|
1 |
FC Barcelona |
21 |
17 |
3 |
1 |
57 |
13 |
44 |
54 |
|
2 |
Atletico Madrid |
21 |
17 |
3 |
1 |
52 |
14 |
38 |
54 |
|
3 |
Real Madrid CF |
21 |
17 |
2 |
2 |
60 |
21 |
39 |
53 |
|
4 |
Athletic Bilbao |
21 |
13 |
3 |
5 |
41 |
27 |
14 |
42 |
|
5 |
Villareal |
21 |
11 |
4 |
6 |
39 |
22 |
17 |
37 |
|
6 |
Real Sociedad |
20 |
9 |
6 |
5 |
38 |
30 |
8 |
33 |
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kwenye Mechi iliyochezwa mapema Jumapili, Atletico Madrid, wakicheza Ugenini, waliichapa Rayo Vallecano Bao 4-2.
Bao kwenye Mechi hiyo zilifungwa na
David Villa, Dakika ya 8, Arda Turan, 30 na 44, na Diego Costa, 75, kwa
upande wa Atletico na Vallecano kufunga Bao zao mbili kupitia Jonathan
Viera Ramos, 40, na Joaquin Larrivey, 76.
VIKOSI:
Barcelona: Valdés; Alves, Piqué, Mascherano, Jordi Alba; Xavi, Busquets, Fabregas; Alexis, Messi, Pedro
Akiba: Pinto, Bartra, Afellay, Tello, Adriano, Sergi Roberto, Dongou.
Malaga: Willy; Angeleri, Sánchez,Flávio, Antunes; Juanmi, Camacho, Tissone, Duda; Pérez, Santa Cruz
Akiba: Kameni, Portillo, Pedro Morales, Eliseu, Pawlowski, Casado, Darder.
LA LIGA
MATOKEO:
Ijumaa Januari 24
Celta de Vigo 4 Real Betis 2
Jumamosi Januari 25
Real Madrid CF 2 Granada CF 0
Real Valladolid 1 Villarreal CF 0
Valencia 2 RCD Espanyol 2
Sevilla FC 2 Levante 3
Jumapili Januari 26
UD Almeria 1 Getafe CF 0
Osasuna 1 Athletic de Bilbao 5
Rayo Vallecano 2 Atletico de Madrid 4
FC Barcelona 3 Malaga CF 0
Jumanne Januari 28
Real Sociedad v Elche CF

No comments:
Post a Comment