Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta ameeleza, kufurahishwa
na ushiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hapo jana
nchini humo.
Rais Keïta ametangaza hayo akiwa mjini Bamako na
kuongeza kuwa, hivi sasa taifa la Mali limesimama kwa miguu yake.
Rais huyo amesema kuwa, uchaguzi wa bunge utasaidia
kuimarisha hali ya amani nchini Mali.Jana wananchi wa Mali walipiga kura kuwachagua
wawakilishi wao wa Bunge wanaowania viti 147, ambapo jumla ya wagombea elfu
moja walijitokeza kuwania viti hivyo.
Karibu watu milioni sita na laki tano, walikuwa
wametimiza masharti ya kupiga kura.Baadhi ya duru za habari zimeripoti kuwepo ushiriki
mdogo wa wapiga kura katika baadhi ya maeneo kutokana na kuwepo vitisho vya
kutokea miripuko ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment