SAFARI ya Arsenal
kuelekea katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa barani Ulaya inaweza kuonekana kama rahisi kutokana na mchezo
wa nyumbani dhidi ya Olympique Marseille baadae leo lakini wameonywa
kuchukulia mchezo huo kwa umakini.
Arsenal ndio wanaoongoza kundi F
wakiwa na alama tisa katika mechi nne walizocheza, wakiwa sambamba na
Napoli waliopo katika nafasi ya pili na Borussia Dortmund waliopo katika
nafasi ya pili. ![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCegYypdVa3qRcDiorQPjRGj9rGknhVk14j-ebqW0ep4J5MN4QREeLuwCTFAHBZPLJ3CWyG3GoVtzx9D5ut4FRpf5BRrv7yhjENXyAhsvj81R9ORtfOCypX9SCvyCUY-kcC9-8NfHn8GkH/s640/2.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCegYypdVa3qRcDiorQPjRGj9rGknhVk14j-ebqW0ep4J5MN4QREeLuwCTFAHBZPLJ3CWyG3GoVtzx9D5ut4FRpf5BRrv7yhjENXyAhsvj81R9ORtfOCypX9SCvyCUY-kcC9-8NfHn8GkH/s640/2.jpg)
Kama Arsenal ikifanikiwa kuifunga Marseille na Dortmund
wakishindwa kuifunga Napoli, kikosi cha Arsenal Wenger kitakuwa
kimekata tiketi ya kucheza hatua hiyo huku wakiwa wamebakiwa na mchezo
mmoja.
Pamoja na hayo kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla ameonya kuwa
hawapaswi kudharau mchezo hata kama Marseille hawataweza kufuzu hatua
hiyo. Cazorla amesema hata kama Marseille hawajapata alama yoyote katika
kundi lao lakini wataufanya mchezo huo kuwa mgumu kwao kwasababu hawana
cha kupoteza.
No comments:
Post a Comment