Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH)
Rai hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Dk. Jullieth Kabengula, wakati akipokea zawadi za vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaosumbuliwa na saratani.
Watoto hao wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoka Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Tanzania 50 Plus Campaign,Dk. Kabengula alisema kumekuwa na tabia ya kudharau mambo yanayoonekana ni madogo kwenye jamii kama vile magonjwa, kwa kuyachukukulia hayana madhara, lakini ukweli ni kwamba yana madhara makubwa kama hayakudhibitiwa mapema.
“Utakuta mzazi anamuona kabisa mtoto wake akiwa labda na kipele kisicho cha kawaida, au kidoa kwenye jicho na anaendelea kukaa naye tu nyumbani badala ya kumfikisha hospitali kwa ajili ya uchunguzi.
Sasa wengi wao wanajitokeza baada ya kuona hali hiyo inaendelea kukua na wakiwaleta tunapowachunguza tunagundua ni saratani, lakini inakuwa imeshaleta madhara makubwa,” alisema Dk. Kabengela.
Zawadi hizo ambazo ni pamoja na kompyuta mpakato (laptop), peni, madaftari, vitabu, mafuta ya kupaka, mikeka, vifaa kwa ajili ya kujifunzia kusoma na kuandika pamoja na vyandarua, vilikabidhiwa na Mwenyekiti na mwanzilishi wa taasisi ya Tanzania 50 Plus Campaign, Dk. Emmanuel Kundis.
Dk. Kundis ambaye aligundulika kuwa ana saratani ya tezi 2004 alisema kuwa watoto hao wana mahitaji mengi, kwa kuwa wengi wao wamekuwa hospitalini hapo kwa muda mrefu sana, na kwamba jamii inahitaji elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa wa saratani ili kuacha kuishi maisha hatarishi.
SOURCE:NIPASHE
No comments:
Post a Comment