WANASIASA hapa nchini, wamepewa somo la kuacha kujikweza, kujilimbikiziamali, kupenda rushwa na matendo yanayopoteza utu wa Watanzania, huku wakijipambanua kuwa wanamuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
![]() |
| Ayati baba wa taifa Mwl:Julius K.Nyerere |
Wito huo umetolewa na Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu, Serengeti mkoani Mara, Alois Magabe katika mahubiri yake ya Misa ya Kumbukumbu ya Miaka 14 ya tangu kufariki dunia kwa muasisi huyo wa taifa.Amesema kuwa Mwalimu aliyapiga vita matendo hayo na kwamba wanasiasa wanaojifanya kuwa wanamuenzi wakati wakifanya hayo ni wanafiki.Paroko huyo amesema kuwa hivi sasa watu wanalalamikia vitendo vya rushwa, uroho wa madaraka na kukosekana kwa miiko ya utumishi, lakini hakuna, hatua zinazochukuliwa. Paroko Magabe amesema Watanzania wakiwa na elimu watasaidia kupambanua mambo na kukabiliana na maadui watatu aliowataja Mwalimu Nyerere, kuwa ni, ujinga maradhi na umaskini ambao sasa umekithiri miongoni mwa wananchi.

No comments:
Post a Comment