Waasi
wa zamani wa renamo nchini msumbiji wamesema kuwa, makubaliano ya amani
yaliyowekwa mwaka 1992 kati ya kundi hilo na serikali ya msumbiji
yamevunjika, baada ya majeshi ya serikali kushambulia ngome za waasi hao wa
zamani wa msumbiji.
Msemaji
wa renamo fernando mazanga amesema kuwa, viongozi wa ngazi za juu wa renamo wanafikiria
pia uwezekano wa kususia uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika
mwezi ujao, iwapo hayatafanyika mabadiliko ya kimsingi kwenye sheria za
uchaguzi nchini humo.
Matamshi
ya msemaji wa renamo yanaashiria uwezekano wa kuanza tena mapigano ya ndani
nchini humo.
Wakati
huohuo, jeshi la msumbiji likitumia vifaru limezingira makao ya afonso dhlakama
kiongozi wa renamo yaliyoko katika eneo la satunjira.
Inafaa
kuashiria hapa kuwa, waasi wa zamani wa renamo kwa muda wa miaka 16 walikuwa wakipambana
na majeshi ya serikali ya msumbiji, hadi yalipofikiwa makubaliano ya amani
mwaka 1992.

No comments:
Post a Comment