EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 22, 2013

SOPHA SIMBA: WASOMI WAZEMBE NDIO WANAOLALAMIKIA AJIRA NCHINI



Serikali imesema kuwa ni aibu kwa wasomi hapa nchini, kulalamika kukosa ajira serikalini, badala ya wao kuwaajiri wenzao ambao hawana elimu ya kutosha. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, sophia simba, katika viwanja vya manga, mwanjelwa jijini mbeya, alipokuwa akijibu maswali ya wananchi waliokuwa wamejitokeza katika viwanja hivyo.Jibu hilo lilitokana na swali la kijana hacha mapesa, ambaye amesema yeye ni msomi wa chuo kikuu cha teofilo kisanji (teku), aliyehoji kuwa inakuwaje serikali inaendekeza mfumo wa ajira hadi mtu awe na uzoefu.







Sophia, ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuia ya wanawake wa chama cha mapinduzi (uwt) taifa, ameeleza kuwa unyanyasaji wa kijinsia umezidi ambapo mbali na wanaume kuwanyanyasa wanawake, pia wapo baadhi ya wanawake wanaowanyanyasa waume zao kwa kuwapiga.Waziri huyo amesema kuwa ukatili huo umeenda mbali zaidi ambapo baadhi ya wazazi hasa wanawake, wanawapiga watoto, kuwaunguza mikono na kuwakata masikio, hali ambayo amesema si njema katika taifa na ni muhimu sasa jamii ikabadilika na kuachana na ukatili wa namna hiyo.Naye mbunge wa viti maalum, mkoa wa mbeya, dk.mary mwanjelwa, amesema umefika wakati kwa vijana kupima kwa hoja za ushawishi wa baadhi ya wanasiasa wasioutakia mema uchumi wao na kutokukubaliana nao.

No comments:

Post a Comment