Mfuko
wa watoto umoja wa mataifa (unicef) umetangaza kuwa, karibu watoto milioni moja
na nusu wa madagascar wanashindwa kwenda shuleni kutokana na umasikini na
mgogoro wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni.
Mwakilishi
wa unicef nchini madagascar stephen lauwerier amesisitiza kuwa, katika mwaka 2008
na kabla ya kuanza mgogoro wa kisiasa nchini humo, jumla ya watoto milioni nne
walikuwa wakisoma katika shule za msingi nchini humo. Taarifa
hiyo ya unicef imetolewa zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika
uchaguzi wa rais nchini humo.
Imeelezwa
kuwa, uchaguzi wa rais nchini humo umepangwa kufanyika siku ya ijumaa oktoba 25
mwaka huu. Waangalizi
wa uchaguzi kutoka umoja wa afrika walioko hivi sasa nchini humo, wataendelea
kubaki nchini madagascar kwa muda mrefu zaidi hata baada ya kutangazwa matokeo
ya uchaguzi huo, ili kuhakikisha amani na utulivu unarejea nchini humo.


No comments:
Post a Comment