EBENEZA MARCH 9 2014

SWACO

royal

tt

NIMO

mvuto
Saturday, October 19, 2013
UGANDA YACHUKUA TAHADHARI KWA MASHAMBULIO YA KIGAIDI
Polisi nchini Uganda imetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea kwa mashambulio ya kigaidi nchini humo, kama yale yaliyotokea nchini Kenya mwezi uliopita.
Taarifa ya polisi ya Uganda imebainisha kwamba, kutokana na kuweko tishio la mashambulio ya kigaidi, vikosi vya usalama nchini humo vimewekwa katika hali ya tahadhari na kwamba, vinafuatilia kwa karibu kila harakati inayotia shaka.
Hatua hiyo ya tahadhari ya vikosi vya usalama nchini Uganda inakuja siku chache tu, baada ya Marekani kupitia ubalozi wake mjini Kampala, kuonya juu ya uwezekano wa kutokea mashambulio kama yale ya mwezi uliopita ya jengo la maduka ya biashara la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.
Watu wasiopungua 67 waliuawa katika shambulio la mwezi uliopita kwenye jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Uganda imekuwa ikiandamwa na vitisho vya wanamgambo wa al-Shabab wa Somalia kutokana na kupeleka majeshi yake huko Somalia chini ya mwavuli wa Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment