EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 19, 2013

KENYATA ASEMA KENYA SASA SHWARI WATALII KARIBUNI



Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewahakikishia usalama watalii wanaoitembelea nchi hiyo ya Afrika Mashariki, kwani serikali yake imechukua hatua za kuimarisha usalama na amani katika maeneo ya watalii.
Rais Kenyatta amebainisha kwamba, vikosi vya usalama vya Kenya vimeimarisha usalama na vimejiandaa kikamilifu kukabiliana vilivyo na tishio lolote lile la ugaidi nchini humo. 
raisi wa kenya Uhuru kenyata

Rais huyo wa Kenya amesisitiza kwamba, maafisa usalama wa nchi hiyo wakiwa na lengo la kuzuia shambulio lolote la kigaidi katika maeneo ya utalii nchini humo, wamechukua hatua mpya za kuimarisha usalama.
Amesema kuwa wote tunashuhudia, 

 ugaidi unaweza kuwa kikwazo cha ustawi na kuimarika sekta ya utalii, kwa msingi huo ni lazima tuchukue hatua za lazima kwa ajili ya kudhamini amani na usalama wa watalii katika nchi yetu.Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kwamba, vikosi vya usalama vya Kenya viko katika hali ya tahadhari kamili ya kukabiliana na tishio lolote lile la usalama ili nchi hiyo iwe na mazingira salama kabisa.
 

No comments:

Post a Comment