Walimu
wametakiwa kupunguza adhabu za viboko kwa wanafunzi, na kuwapa adhabu nyingine
mbadala kwani viboko peke yake sio suluhu la kumrekebisha mwanafunzi.
Akizungumza
na mwandishi wa kituo hiki mapema hii leo ofisini kwake mkuu wa shule ya msingi
ligula mwalimu tumaini mwangata amesema kuwa kumchapa mwanafunzi ni kumuondolea
hadhi yake na kumfanya kuwa na nidhamu ya woga.Pia amesema kuwa kumpunguzia
mwanafunzi adhabu ya viboko kunajenga mahusiano mazuri kati yake na mwalimu na
kumfanya awe anasikiliza na kuelewa kile mwalimu anachomfundisha.Hata hivyo
amewataka wazazi kusaidiana na walimu kwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao
pamoja na kulipa michango mbalimbali ya shule na kuhudhuria katika vikao
mbalimbali vya shule vinavyolenga kujadili mwenendo wa watoto wao.

No comments:
Post a Comment