MTWARA-
NA:kassim Ngumbi
Watahiniwa wa kidato cha pili katika shule ya sekondari
ya Aman Islamic iliyoko katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, wameishukuru
serikali kwa kurudisha mitihani ya kidato cha pili mashuleni.
Hayo yamesemwa na mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Juma
Yussuf alipokuwa akizungumza na mwandishi wa pride fm radio shuleni hapo mapema
hii leo, ambapo amesema kuwa kurudishwa kwa mitihani ya kidato cha pili
mashuleni, kutasaidia wanafunzi kujijengea mazoea ya kujisomea mara kwa mara
kwa lengo la kufanya mitihani hiyo.
Amesema kuwa mitihani hiyo ya kidato cha pili
itaongeza umakini kwa wanafunzi katika kufuatilia masomo yao, na itasaidia kuwa
na wanafunzi wenye kujiamini na kujitambua kuwa wao ni wanafunzi, kwani mara
nyingi ukuaji wa vijana huanzia kipindi ambacho wapo mashuleni.
Pia Juma amesema kuwa, wanashukuru kutokana na
maswali mengi yanayotungwa katika mitihani hiyo yanaendana na masomo ambayo
tayari yamekwishafundishwa, huku pia upande wa usimamizi ukiwa wa kawaida,
ambapo wanatarajia kumaliza mitihani hiyo Ijumaa ya Oktoba 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment