WAZAZI na walezi mkoani Mtwara wamekumbushwa kutunza
na kulinda matumizi bora ya miundombinu ya elimu inayotolewa na wafadhili kwa
watoto wao, ili kuifanya iwe endelevu na kumsaidia mwanafunzi kujifunza na kuwa
na ubora wa ufaulu.
![]() |
| wazili wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa MH: AWA GHASIA |
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Hawa Ghasia, wakati
wa ugawaji wa msaada wa Taa za nguvu ya solar katika kata ya Dihimba, kwa wanafunzi
wanaosoma katika shule nne za msingi kutoka katika kata hiyo.
Waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mtwara
Vijijini, amewahimiza wazazi na walezi hao kuwasimamia na kuhakikisha watoto
hao wanazitumia taa hizo kwa lengo la kujisomea, kutokana na elimu kuchukua
wigo mpana katika kujiletea maendeleo endelevu.
Msaada huo uliotolewa na Hotel ya Double Tree kutoka
jijini Dar es salaam wenye jumla ya Taa za solar 200, umelenga kuwasaidia
wanafunzi wanaosoma darasa la sita kwa ajili ya kujisomea wakati wakijiandaa
kuingia darasa la saba, kwa lengo la kuongeza ubora katika kujisomea na
kuongeza ufaulu.
![]() |
| WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MKOANI MTWARA |
Waziri Ghasia amesema kuwa msaada huo umezinufaisha shule
nne za kata ya Dihimba, ambazo ni Dihimba yenyewe iliyopata taa 104, shule ya
msingi Namanjele taa 39, Muungano taa 27 na Miuta taa 30.
Awali akizungumza katika makabidhianao hayo
mkurugenzi wa mauzo wa Hoteli ya Double Tree Florenso Kirambata, amesema kuwa dhumuni
hasa ni kuwelimisha wanafunzi chanzo kingine cha umeme kupitia taa hizo, ambazo
zinaweza kutumika kwa masaa manne na kudumu kwa miaka kumi.


No comments:
Post a Comment