EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 22, 2013

RAISI JOYCE BANDA WA MALAWI ATISHIWA KUUAWA



Rais joyce banda wa malawi ametishiwa kuuawa, baada ya kutekeleza mikakati yake ya kufichua na kupambana na ufisadi uliokithiri nchini humo.
Waziri wa habari wa malawi brown mpinganjira, amethibitisha habari hizo na kusema kuwa, mafisadi wameanza kutishia maisha ya kiongozi huyo wa malawi, kutokana na msimamo wake wa kuvunja baraza la mawaziri na kufichua ufisadi mkubwa wa kifedha uliofanywa na viongozi waandamizi nchini humo. 
 
Raisi wa malawi Mh Joyce Banda
Mpinganjira amesema kuwa, baadhi ya vitisho hivyo vimetolewa toka nje ya nchi hiyo na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na hatimaye kubaini wahusika wa njama hizo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 10 oktoba mwaka huu, rais joyce banda aliamua kulivunja baraza la mawaziri baada ya kufichuliwa kwa kashfa ya ufisadi wa dola milioni tatu, uliofanywa na viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya malawi.  Joyce banda anayehesabiwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo, aliingia madarakani mwaka 2012 baada ya kufariki dunia bingu wa mutharika rais wa zamani nchini humo.

No comments:

Post a Comment