EBENEZA MARCH 9 2014
SWACO
royal
tt
NIMO
mvuto
Wednesday, October 9, 2013
KENYA NA TANZANIA ZAESABU SENSA YA PAMOJA
NA: MGENI ISMAIL
Kenya na Tanzania hapo jana zimeanza kufanya sensa ya pamoja ya tembo na wanyama wengine wakubwa, kwa kutumia ndege katika eneo la Amboseli na Kilimanjaro Magharibi.
Mamlaka ya wanyamapori ya Kenya imesema kazi hiyo ya wiki moja, ina lengo la kufahamu hali ya wanyamapori katika eneo ambalo wanyama hao huvuka mpaka wa nchi hizo mbili.
Kazi hiyo pia itahusu kufahamu idadi halisi ya wanyama, na maeneo waliko wanyama hao na mazingira wanayoishi.
Sensa hiyo itakayogharimu dola za kimarekani laki 1.4, inagharamiwa kwa pamoja kati ya Kenya na Tanzania.
Mara ya mwisho sensa hiyo ilifanyika mwaka 2012, ambapo idadi ya wanyama ilionekana kuwa katika hali ya kawaida isipokuwa idadi ya tembo ilipungua kiasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment