Katika Mechi hiyo, Pantilimon, anaetoka
Romania, aliokoa Bao mbili na kuiwezesha Man City itoke kwenye Mechi
bila kufungwa Bao katika Mechi ya kwanza baada ya Mechi 7.
Joe Hart ndie Kipa Nambari Wani wa Man
City lakini Kipa huyo ambae pia ni Nambari Wani kwa England amekuwa
akifanya kosa baada ya kosa katika Mechi zake Msimu huu.
Na Pellegrini ametamka: “Kipa yeyote
atakaecheza atakuwa na sapoti yangu. Costel kawaida anacheza Mechi za
Makombe ya Ligi na FA na Mechi na Newcastle ilikuwa muhimu kwake.”
Alipobanwa aweke waziwazi nani atakuwa Kipa Jumamosi, Pellegrini alijibu: “Nimeshakwambia nitafikiria hilo Alhamisi.”
No comments:
Post a Comment