EBENEZA MARCH 9 2014

SWACO

royal

tt

NIMO

mvuto
Saturday, October 19, 2013
ETHIOPIA YATUHUMIWA KUWATESA WATUHUMIWA WA KISIASA
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, watuhumiwa wa kisiasa nchini Ethiopia wamekuwa wakiteswa.
Taarifa ya Human Rights Watch inaonesha kuwa, maafisa wa magereza nchini Ethiopia wamekuwa wakiwatesa mahabusu wa kisiasa wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali ili wakiri kwamba, wamehusika na vitendo wanavyotuhumiwa navyo au hata makosa ambayo hawajayafanya.
Baadhi ya watu waliokuwa wakishikiliwa katika kituo cha kikosi cha kupambana na makosa ya jinai mjini Addis Ababa cha Maekelawi wanasimulia kwamba, mahabusu katika kituo hicho wamekuwa wakiteswa kwa kutumia vifaa mbalimbali.
Wamesema kuwa, miongoni mwa mateso hayo ni kupigwa au kufungwa miguu juu kichwa chini na kuachwa katika hali hiyo kwa masaa kadhaa.
Taarifa ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch imebainisha kwamba, tangu kufanyika uchaguzi mkuu nchini Ethiopia mwaka 2005 uchaguzi ambao ulizua makelele mengi, serikali ya Addis Ababa imekithirisha mbinyo dhidi ya uhuru wa kujieleza, huku sheria ya kupambana na ugaidi iliyopasishwa mwaka 2009 ikiipa uwezo zaidi serikali wa kuwakandamiza wapinzani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment