EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 19, 2013

NKOSAZANA ZUMA KUFANYA ZIARA KONGO WIKI HII



Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Nkosazana Dlamine Zuma anatarajia kufanya ziara mwishoni mwa juma hili nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, katika mpango wa kuchochea uwiano wa mashariki ya nchi hiyo.
 
Raisi wa AU NKOSAZANA ZUMA
Nkosazane Dlamini Zuma anafanya ziara hiyo chini ya mualiko wa serikali ya rais Joseph Kabila kuanzia Octoba 20 hadi 22.
Ziara hiyo ya kwanza ya kiongozi huyo wa juu wa Umoja wa Afrika, inakuja kufuatia makubaliano yaliofikiwa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, Februari 24 mwaka 2013 chini ya viongozi 11 wa mkutano wa

 viongozi wa nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, DRCongo inatakiwa kufanya mageuzi ya ndani kuhusu idara za usalama na mabadiliko ya kisiasa, hususan swala linalozua utata la kutoa madaraka zaidi kwa mikoa.
Aidha nchi nyingine kumi zilizo saini mkataba huo, zilijikubalisha kutovumilia na kutotoa msaada wa aina yoyote kwa makundi yanayo yumbisha usalama wa taifa hilo tangu miongo miwili.
Mataifa ya Rwanda na Uganda majirani ya DRCongo ni miongoni mwa mataifa yaliosaini mkataba huo.
Umoja wa Mataifa unayatuhumu mara kadhaa mataifa hayo kutoa msaada kwa kundi la waasi wa M23 wanaopambana na majeshi ya serikali ya taifa hilo ya FARDC tangu mwezi Mei mwaka 2012 katika mji wenye utajiri wa madini wa kivu ya Kaksazini, tuhuma ambazo srikali ya Kigali na Kampala zinatupilia mbali.

No comments:

Post a Comment