S

Wakati Serikali imeeleza nia yake
ya kuangalia upya utozaji wa kodi ya kila mwezi kwenye laini za simu za
mkononi, imeeleza pia mpango wa kufunga mtambo maalumu ili kubaini
malalamiko ya kampuni za simu kudaiwa kuiba fedha za watumiaji.
Katika kile
kinachoonesha kusikiliza kilio cha wananchi, Serikali imesema inapitia
maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau ili kuiangalia upya sheria
hiyo ya kutoza kodi ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa nia ya kuwapunguzia
wananchi mzigo huo.
Serikali imetoa kauli hiyo Dar es Salaam jana
kupitia kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame
Mbarawa na Waziri wa Fedha, Dk ...
No comments:
Post a Comment