SUALA la
nafasi ya meya wa jiji la Arusha limechukua sura mpya, baada ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kudai kuwa sio ajenda yao ya sasa.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Katibu wa Kanda ya Kaskazini wa CHADEMA, Amani
Golugwa, alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa kwamba
kwa sasa madiwani wa chama hicho wamejipanga kuweka mikakati madhubuti
ya kupanga na kusimamia miradi ya maendeleo iliyo kwenye halmashauri
hiyo kwa ushirikiano wa karibu na wananchi kwa manufaa ya taifa.
Alisema
pamoja na ukweli kuwa taratibu zilizotumika kumweka Meya Gaudence Lyimo
madakani hazikuwa sahihi, lakini kwa sasa kipaumbele chao ni
kushughulika na maendeleo ya wananchi.
Suala la nafasi ya meya wa jiji hili, lilisababisha maafa makubwa wakati chama hicho kilipopinga kanuni zilizomweka madarakani.
Katika hatua
nyingine, CHADEMA imemtaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kuacha unafiki wa kupinga kodi ya sh 1,000
kwa kila laini ya simu wakati wabunge wa chama chake ndiyo
walioipitisha.
Golugwa
alisema kuwa kodi hiyo ilipitishwa kwa kishindo na wabunge wa CCM ambao
ni wengi wakati wale wa CHADEMA walipokuwa kwenye maombolezo ya wananchi
wanne waliouawa kwa bomu jijini Arusha, hivyo haiwezekani leo CCM
kuikataa.
“Tunamsihi
Nape aache unafiki; awe mkweli, haiwezekani wabunge wa chama chake
wapitishe kodi hii inayowaumiza wananchi hasa wa kipato cha chini halafu
yeye akimbilie kwenye vyombo vya habari kuipinga. Kama CCM ilikuwa
haikubaliani na kodi hii isingepitishwa bungeni.
Nape
anatakiwa aache usanii wa kujifanya hakujua tozo hii ya laini za simu
wakati ina baraka ya baraza la mawaziri ambalo linaongozwa na Mwenyekiti
wao wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, na limepitishwa na wabunge wa chama
chake sasa anataka kuwahadaa wananchi kuwa CCM haihusiki,” alihoji
Golugwa.
Alisema kuwa
tayari CHADEMA imeshaanza mchakato pamoja na wabunge wake ili kuona
namna suala hilo litakavyoshughulikiwa ikibidi hata kwa kupeleka hoja
binafsi bungeni ili kuhakikisha kodi hiyo inayowaumiza wananchi walio
wengi inaondolewa.
Kauli ya
Golugwa imekuja siku chache baada ya Nnauye kutoa msimamo wa CCM
kuipinga kodi hiyo na kuishauri serikali kuiondoa na itafute njia
nyingine ya kuongeza mapato ambapo mamlaka ya mapato nchini (TRA)
imesema kwamba itakuwa inakusanya bilioni 28 kwa mwezi kwa kukata sh
1,000 katika kila laini ya simu. Inasemekana kuwa Watanzania wanaotumia
simu sasa nchi nzima ni zaidi ya mil. 28.
Baraza lataka Katiba ya Tanganyika
BARAZA
la Katiba la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) linatarajia
kutoa mapendekezo yake leo ya uundwaji wa Katiba mpya, huku likitaka
kusitishwa kwa mchakato huo hadi hapo katiba ya Tanganyika
itakapopatikana.
Hilo
ni moja ya maazimio yaliyofikiwa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa
kupitia kipengele kimoja baada ya kingine ndani ya rasimu ya Katiba mpya
kulikofanywa na wajumbe wa baraza hilo wapatao 70 kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini.
Felix
Nielema, mwanaharakati kutoka Wilaya ya Ngara, alisema rasimu hiyo
inazungumzia muungano, hivyo kufanya iwe batili, kwani inawalazimisha
Watanzania kuingia kwenye muungano bila ya kuwa na katiba yao.
“Jamani
katika hili tunatakiwa tuwe makini sana, kwani hawa jamaa tayari
wanatulazimisha kuingia kwenye mambo ambayo hatujashirikishwa. Hivyo
rasimu hii isimamishwe kwanza, tupate kwanza katiba ya Tanganyika ili
tukija kujadili suala la muungano tujue yapi yaingizwe katika muungano
na yapi yaachwe,” alisema Nielema.
Wakili
Frugence Masawe, alikosoa sura ya 10 ndani ya rasimu hiyo inayoelezea
mambo ya mahakama ya muungano wakati ukweli ni kwamba suala la mahakama
si la muungano.
Naye
Mwangalizi wa Haki za Binadamu kutoka Ukerewe, Benjamin Mtebe, alisema
katika kipengele cha uendeshaji wa Bunge, kinaeleza kwamba endapo hoja
ya bajeti ya wizara fulani itapingwa na wabunge na kurudishwa kwa ajili
ya marekebisho, ikipingwa tena kwa mara ya pili serikali ina uhalali wa
kuipitisha hivyo hivyo.
Kutokana
utaratibu huu, wajumbe waliokuwa wakijadili kipengele hicho
walipendekeza kuwa ni vema bajeti ikarekebishwa hata mara sita mpaka
wabunge watakapoiridhia, kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi.
Awali
Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia, alisema baraza hilo
limepewa kibali halali na Tume ya Kurekebisha Katiba kuichambua rasimu
ya Katiba mpya.
Ndugu wanahabari, kwanza
kabisa napenda kuwashukuru kwa kuitikia wito wangu, ili niweze kuzungumza na
watanzania kupitia kwenu kuhusu hatari kubwa inayolikumba taifa ya madawa ya
kulevya.
Biashara haramu ya dawa za kulevya imekua kwa kasi sana hapa nchini miaka ya hivi karibuni licha ya kuwa na vyombo lukuki vya ulinzi na usalama na licha ya kuwa na Tume maalumu ya kudhibiti madawa ya kulevya chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera Uratibu na Bunge Mhe. Wiliam Lukuvi tarehe 26 Juni, 2013 siku ya maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya huko Dodoma ni kwamba katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012 watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini. Aidha, watanzania wapatao 240 walikamatwa na madawa ya kulevya katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika ya kusini na hivyo kutia doa taswira ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa. Kutokana na kukithiri kwa biashara hii haramu, Serikali kupitia maadhimisho hayo ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya duniani ilitangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya kuwa ni janga la taifa.
Mtakumbuka pia kwamba hivi majuzi, muda mfupi baada ya Serikali kutangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya ni janga la taifa , walikamatwa wasichana wawili ambao ni watanzania huko Afrika ya kusini wakiwa na kilo 150 za madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya randi milioni 42.6 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 6 za kitanzania.
Ndugu wanahabari, matukio yote haya yametokea ndani ya kipindi cha miaka sita tu ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne ambapo kuna viongozi wa juu Serikalini ambao waliwahi kusema kuwa wanawajua watu wanaojishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya lakini mpaka sasa hawajawataja wahusika na wala hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wahusika.
Ndugu wana habari, miongoni mwa viongozi wa serikali na taasisi nyingine waliosema kuwa wanawafahamu wafanya biashara ya madawa ya kulevya ni:-
Rais Jakaya Kikwete, ambaye alipiga hatua kubwa zaidi na kusema anawajua hata viongozi wa dini wanaofanya biashara hiyo. Licha ya maaskofu na viongozi wengine wa dini kumtaka Rais awataje wahusika hao wa madawa ya kulevya ili kuuweka ukweli wazi, Rais hajafanya hivyo mpaka sasa.

Kamishna
wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya: huyu alisema anayo majina ya vigogo (kwa maana ya viongozi)
wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini hajaweka majina hayo
hadharani na wala haijulikani kama wahusika hao wamechukuliwa hatua yoyote hadi
sasa.
Mbunge wa Mwibara – Kange Lugola alisema katika bunge la bajeti 2013/2014 kuwa kama Rais na Kamishna wa tume ya kudhibiti dawa za kulevya wanawajua “kwa majina” watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya na hawataki kuwataja watu hao wala kuwachulia hatu yamkini watu hao ni miongoni mwa mawaziri ndio maana kuna kigugumizi cha kuwataja na kuwachukulia hatua. Tangu Mhe. Kange Lugola alihusishe baraza la Mawaziri na kashfa hiyo ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya hakuna hatua yoyote ilivyochuliwa na Serikali kuthibitisha au kubatilisha kauli hiyo.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi aliwahi kutoa taarifa ya wazi kuwa kuna kundi la matajiri wanaoshirikiana na viongozi wa Jeshi la Polisi waliokuwa wanapanga njama za kumwekea mtoto wake dawa za kulevya ili wambambikizie kesi ya dawa za kulevya na hivyo kuchafua heshima ya Bw. Mengi na familia yake. Ndugu mengi alisisitiza katika taarifa yake kwamba yuko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na mamlaka nyingine zinazohusika ili kubaini njama hizo na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika lakini mpaka leo Ndugu Mengi hakuhojiwa ili kuthibitisha kauli yake jambo linaloashiria kwamba kuna ukweli katika kauli yake.
Baada ya matukio yote haya na baada ya Serikali kukaa kimya kuhusu matukio hayo, mimi kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ninatoa tamko kama ifuatavyo:
Rais Jakaya Mrisho Kikwete awataje na kuwachukulia hatua watu aliosema anawafahamu wanaojishughulisha na biashara ya dawa za kulevya la sivyo akubali kubeba shutuma kwamba Serikali yake ndio Mratibu Mkuu wa biashara ya dawa za kulevya ndio maana anashindwa kuchukua hatua.
Kamishana wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya awajibike kwa kutoa maelezo kwa umma juu ya hatua alizochukua dhidi ya wahusika wa biashara ya dawa za kulevya aloiosema anawafahamu la sivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italazimika kuwashawishi wananchi kuamini kwamba yamkini na yeye yumo katika mtandao wa wafanya biashara haramu ya dawa za kulevya ndio maana anasita kuwachukulia hatua wahusika hao ambao alishakiri kuwa anawafahamu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege awajibike kwa kutoa maelezo kwa umma kuwa ni tatizo gani linaloikabili mamlaka yake hadi kufanya viwanja vya ndege vya Tanzania kuwa ndio njia rahisi ya kuingiza na kusafirishia madawa ya kulevya katika ukanda wa Afrika Mashariki?
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi wawajibike kwa kutoa maelezo kwa umma kuwa ni kazi ipi wanayofanya ikiwa madawa ya kulevya yanaingizwa nchini na kusafirishwa nje ya nchi kwa kasi kubwa zaidi?
HITIMISHO: Ni vema kama taifa tukatambua madhara ya madawa ya kulevya kwa vijana wetu ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Kupuuzia na kutochukua hatua kwa wahusika wa dawa za kulevya ni kuangamiza nguvu kazi ya taifa. Nguvu kazi ya taifa ikishaharibiwa na dawa za kulevya hatuna taifa tena. Hivyo Serikali ifahamu kwamba kuendelea kulifumbia macho jambo hili kwa manufaa ya mafisadi wachache ni kulihujumu taifa na huo ni usaliti dhidi ya kiapo ilichokula cha kulitumikia taifa na kusimamia usitawi wa wananchi wa Tanzania. Aidha, Serikali itambue pia kwamba kuendelea kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote juu ya jambo hili kunatoa dalili kwamba yamkini ya yenyewe inahusika na biashara hiyo.
MUHIMU: IKIWA SERIKALI ITAENDELEA KUPUUZIA JAMBO HILI AMBALO LINALIANGAMIZA TAIFA, BASI KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI ITAENDESHA OPERESHENI NCHI NZIMA ILI WANANCHI WAPIGE KURA KWA WAHUSIKA WAKUU WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, NA BAADA YA ZOEZI HILO, TUTAANIKA HADHARANI (KWA KUWATAJA MAJINA) WAHUSIKA WA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA.

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
NA WAZIRI KIVULI WA MABO YA NDANI YA NCHI
Imetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2013
Imetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2013

No comments:
Post a Comment