![swacotz forum www.kassimngumbi.blogspot.com](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTGrKYOGGk69Qha430HZwP_oyG-9RhR0d2vl08RiRo3O4x1FYpueRoctgH0O_iFnXk-zXqW4yaUNDoOBJF2086QMkF-LsLzGGf_PW9zbNfglsHfSw9H7Q_9dr8Q4SzE3dFgtNRuFr7lD8/s320/tttttttttttttttttfffffffffffffff.jpg) |
Rais wa TFF Leodiga Chilla Tenga |
Chama cha mpira wa miguu nchini TFF kimeonekana kutatanisha na kuwachanganya wananchi na wadau wa soka la Tanzania kutokana na kauli yake iliyoitoa mapema hapo jana kuwa wamepanga kujadili masuala yahusuyo katiba inayoiongoza chama hicho Tar:13 July siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania taifa starz itakuwa ikikipiga na timu ya taifa ya Uganda The Cranes katika mchezo wa kuwania kufudhu kushiriki katika michuano ya Afrika inayoshirikisha wachezaji wanaoshiriki ligi la ndani.
![swacotz forum www.kassimngumbi.blogspot.com](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9MUTjZ6oKA7DXr3Y02Tpeq_bEZ66sdOgmDbTN_RRSdIOUKfmw_FFOH9XeiakX06cuK1FHlFGJsKfKeaTZ-inyIe05seGyA5c8XE5yJqGR-wT0uw7lL62qVyUWtJ-6j58aTdSsO8jX7XY/s320/tff.jpg) |
uongoz TFF |
kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa TFF Angetile Hosea Mwalubeja imeonyesha kuamsha hisia za watanzania kwa kutokuwa na imani na upangwji wa ratiba hiyo kwani wanahisi kuwa kuna michezo michafu inataka kufanyika ndani ya TFF kuhusu katiba.Akielezea wasiwasi wake moja kati ya wadau wa soka nchini amadhan Hamisi ama Don King amesema kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF ambao wanatakiwa kuhudhulia kikao hicho pia ni watu muhimu katika kuhudhulia mechi ya starz na Uganda na ni lazima wafanye hivyo kama sehemu ya majukumu yao hivyo basi kitendo cha mambo haya mawili kufanywa siku moja wao wanaona kama njama ya kuwafanya wajumbe hao washindwe kufanya maamuzi yao sahihi kwani watakuwa na haraka ya kuwahi mchezo pia,kitendo ambacho kitawapa mwanya mafisadi wanaorubuni soka la Tanzania kuingiza mikono yao kwa nia mbaya.
No comments:
Post a Comment