![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggR0bwpOoHeIKJkSTrPMBGyj80LnMikvNq-Ko8rK-ktu9ByWE19YfIl5cZ1zRY7QIVLCk_F1Xuz4v-zCZWBMC3JyY9nZ2sy54gtD5EewV76W4T421mrRSAIeVQtqW2-UGG9RDBYZyYXkY/s320/yanga.jpg) |
yusuph manji kushoto mw/kt Yanga |
Uongozi wa klabu ya soka ya dar young African umesema kuwa wamepanga
kufanya kikao kizito na wachezaji wake siku chache zijazo ili kujadili
mustakabali wa klaabu hiyo katika kujiandaa kuelekea msimu mpya wa ligi
kuu soka Tanzania bara2013-2014.
![swacotz forum www.kassimngumbi.blogspot.com](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifAdM9eVG5CBy2qABNsVnNxIAEinsZfRaJehxtDCXTAHfMdzFYG8Q2DYaT7ZQTrClpjeZ225D-367J_7-sFl3VcMzz3O_VhTibgHXa-K-Hlmzxfho-pNHe9O_zYzvWItIbhW7c8RDDvPw/s320/mwalusako.jpg) |
Lawlenc Mwalusako katibu mkuu Yanga |
katibu mkuu wa klabu hiyo Lawlenc Mwalusako amesema kuwa kikao hicho
kinatarajiwa kufanyika mapema mwezi july mara baada ya wachezaji wote
kurejea toka mapumzikoni ambapo wanatakiwa kuripoti klabuni hapo siku ya
tar moja mwezi ujao na kuanza rasmi mazoezi yao siku ya tar mbili mwezi
huohuo july mara baada ya kocha mkuu wa timu hiyo ERnie Brandts kurejea
toka nchini kwao Serbia ambakoo yuko kwa sasa kwa mapumziko ya mwisho
wa msimu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9HC0FkivKoUq7g3SzEnwaD2b7xLQ8xPhAL9x7lJosCnjiOV9k6rIBTdT7vdaLjRpocew4qMyPmPnJ8Ba3PrJ2HESv3uzu6wajwFvql6DlFrUqK5OG1bjHaK1exI5OMRNpTUqI7GpcMlQ/s320/kocha+yanga.jpg) |
Ernie Brandts-kocha mkuu Yanga |
katika taarifa yake Mwalusako amesema kuwa kikao hicho kinalenga
kinalenga kuzungumzia mikakati na mipango ya klabu yao katika
kuhakikisha wanalinda heshima yao na kutetea ubingwa wa Tanzania bara
ambao wanaushikilia kwa sasa lakini kuhusiana na tarehe Mwalusako
ameeleza kuwa kutapangwa tarehe ya kufanyika kwake mara tu baada ya
Brandts kuingia na kutolewa kwa ratiba ya ligi kuu ambayo ndiyo itakuwa
ni mwongozo wao kuhusu vitu gani wapange kulingana na mechi
watakazopangiwa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8MpiabXVf7dcVI5S1NqNbwVl-pur-UlZ5GmkSYCQu6Bb3Czo3asJhqjvTSO-qIPJelZxw1kPEMUQ7GN4WxI_SHbgwG0C0ShpPY4PRQH4yI4KlO-7G_BxLVheaIR5Lkqn6Xr4tiFJwp9Q/s320/yyyyyyyyyyyyyyaaaaaaaaaaaa.jpg) |
mwalusako kulia |
No comments:
Post a Comment